• CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM CHAMA MAKINI KINACHOFANYA MAAMUZI KWA VIKAO RASMI
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA

Flag this message JENISTA ATOA MSAADA WA PIKIPIKI 10 KWA MAKATIBU KATA WA CCM.


NA DUSTAN  NDUNGURU    SONGEA.

MBUNGE wa jimbo la Peramiho wilaya ya Songea vijijini mkoa wa Ruvuma Jenista Mhagama ametoa msaada wa pikipiki  saba zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa makatibu kata wa chama cha mapinduzi(CCM) ili kuwarahisishia utendaji wa kazi zao ndani ya chama.

Jenista alitoa msaada huo jana katika kijiji cha Lipokela kilichopo katika kata ya Mbingamhalule ambapo kata za Kikunja ,Mtyangimbole,Muungano, Kata mpya ya Peramiho ,Mpandangindo ,Mkongotema ,na Mbingamhalule zilinufaika na msaada huo.

Akikabidhi msaada huo aliwataka makatibu kata hao kutambua kwamba pikipiki hizo walizokabidhiwa siyo mali yao binafsi bali zitatumika kwa ajili ya shughuli zote za chama na serikali ikiwa ni pamoja na kusaidia kubebea wagonjwa katika maeneo yao.

Alisema kuwa kutolewa kwa pikipiki hizo kutaongeza ufanisi wa kazi za chama ambapo makatibu kata watakuwa na uwezo wa kutembelea wanachama wao na kuhamasisha wale ambao hawajajiunga na chama hicho wajiunge ili kuongeza idadi ya wanachama.

Aidha Mbunge huyo pia alitoa msaada wa trekta dogo la kulimia (power tiller) lenye thamani ya shilingi milioni tisa kwa wananchi wa kijiji cha Lipokela kama ahadi yake aliyoitoa wakati wa ziara ya waziri mkuu Mizengo Pinda mkoani Ruvuma mapema mwaka huu.

Naye diwani wa kata ya Mbingamhalule Nasli Nyoni alimshukuru na kumpongeza mbunge huyo kwa michango yake anayoitoa kwa wananchi katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya jimbo hilo ikiwemo  pamoja na jitihada za upatikanaji wa kata mpya ya Mbingamhalule iliyomegwa kutoka kwenye kata ya Magagura.

Katika hatua nyingine Jenista akiwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo lake aliweza kufungua matawi mawili ya chama cha mapinduzi(CCM) likiwemo tawi la Towatowa na Mbinga road kulingana na ongezeko la wanachama.

Akiongea mara baada ya kufungua matawi hayo mapya aliwataka wanachama kuhakikisha wanahamasisha wanachama wengine kujiunga na kwamba chama cha mapinduzi kimedhamiria kutekeleza ahadi zake zilizotolewa kwa vitendo ili kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wake.

                            MWISHO.

This entry was posted in

Leave a Reply