• CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM CHAMA MAKINI KINACHOFANYA MAAMUZI KWA VIKAO RASMI
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA

Na Charles Charles
SITAKI kumjadili mtu mwingine yeyote aliyekikimbia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kisingizio chochote kile katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani baadaye mwaka huu ila nitagusia watu wanane tu.

Hao ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Mbunge wa Segerea jijini Dar es Salaam, Dk. Makongoro Mahanga na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Mgana Msindai.

Wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salalam kati ya mwaka 2007 – 2012, Sajenti John Guninita na aliyewahi kuwa Mbunge wa Nyamagana mkoani Mwanza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha.

Watatu waliobaki ni wabunge waliomaliza muda wao katika bunge lililopita ambao ni Saidi Nkumba wa Sikonge, Tabora; Modestus Kilufi wa Mbarali katika mkoa wa Mbeya na Sioi Sumari aliyewahi kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha mwaka 2012 na kusambaratishwa vibaya.

Wote katika ujumla wao, kila mmoja kwa kinywa chake mwenyewe alijitahidi sana kudai kwa mfano kuwa CCM imepoteza mwelekeo, haitendi haki tena kwa wanachama wake wanaoomba uteuzi wa kugombea urais, ubunge, udiwani na hata vinginevyo.

“Tulitaka tupate dereva ambaye pia ni fundi. Tulitegemea uamuzi wa haki ungetumika, (lakini) bahati mbaya Mwenyekiti wa Chama (au Rais Jakaya Kikwete) alipuuza mawazo ya wananchi”, alisema Mgeja alipokuwa akitangaza kuihama CCM na kwenda Chadema, Alhamisi ya wiki iliyopita.

Hata hivyo, Mgeja ambaye ni mmoja kati ya wafuasi kindakindaki wa Lowassa waliomfuata Chadema alishindwa, angalau tu kidogo kuwataja wananchi waliotoa mawazo na kisha kupuuzwa, na pia hakuweza kuyataja ni yapi kwa sababu alijua kwamba ni muongo.

Mbali na hilo, Mgeja anafahamu namna Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa mkoa wake wa Shinyanga alikokuwa mwenyekiti walivyofuatwa na magari, saa nne za usiku wa Julai 10 kutoka hotelini walikokuwa wamefikia, kisha wakapelekwa nyumbani kwa mbunge mmoja aliyemaliza muda wake kutoka mkoa wa Simiyu ambako, pamoja na mambo mengine walipewa maelekezo ya kufanya vurugu endapo jina la Lowassa lisingewasilishwa kwao, lakini wakayapuuza.

Bila shaka anajua hata vijana waliokuwa wakiandamana ili kushinikiza jina hilo liingizwe katika kile kinachoitwa ‘Tano Bora’ waliahidiwa fedha, na pia baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) waliopelekwa Saint Gasper Hostel Julai 11 walikwenda kuhongwa ili wafanye vurugu ukumbini baadaye mchana huo, lakini walipojaribu wakajikuta wanaumbuka.

Aidha, Guninita aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) hadi mwaka 1996 alipovuliwa vyeo vyote hivyo kwa utovu wa nidhamu, akakasirika na kuhamia Chadema kabla hajarudi na kuhama tena, Alhamisi hiyo akiwa pamoja na Mgeja naye hakubaki nyuma.

“CCM ya sasa imejaa viongozi wenye ubabe, dharau na majivuno. Wanapewa vyeo vya uyoga, wanatukana baba zao”, alisema akiwa anamlenga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Paul Makonda na kuongeza kwamba chama hicho kinachotawala hakina demokrasia.

Sitaki kurejea madai yaliyotolewa na Dk. Mahanga, Msindai na Nkumba kwa sababu ni yaleyale kuwa “CCM haitendi haki”, vinginevyo wanatumia kichaka cha Lowassa kuwa amenyang’anywa haki yake ya kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, madai yanayotengenezwa mezani kwa ajili ya maslahi ya mtu na genge lake.

Hizo ndizo kauli walizotunga na kukubaliana kwamba wazitumie kwa nguvu zao zote ili kuwadanganya Watanzania, lakini hasa wanachofanya ni kueneza uzushi, uongo, upotoshaji na kutumika kwa maslahi ya “Lowassa kwanza”, mambo mengine yanakuja baadaye.

Napenda nijulishe kuwa ukimwondoa Mgeja, wote waliobaki kwa maana ya Dk. Mahanga, Msindai, Guninita, Nkumba, Sioi na Kilufi waliingia kwenye kura za maoni za kutaka kugombea ubunge kwenye majimbo yao, lakini wote wakashindwa na kususia matokeo kwa sababu ya uchu wao wa madaraka.

Pamoja na kuwa Mbunge wa Segerea na pia Naibu Waziri kwa miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2000, Dk. Mahanga ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Serikali ya Awamu ya Nne waliokuwa na ‘gundu’ kwenye majimbo yao.

Alikuwa mbunge anayechukiwa kwa kiasi kikubwa na wapiga kura wa jimbo hilo na kulazimika kubadili njia ya kutoka na kurudi nyumbani kwake, sababu kubwa ikiwa ni kuzomewa katika baadhi ya vijiwe.

Mathalani, waendesha bodaboda wanaoweza kuitwa kuwa “zimepinda” katika lugha ya mjini walifikia mpaka hatua ya kufukuzana na gari lake barabarni huku wakimzomea, hivyo alichofanya ni kutafuta njia anakoweza kupita kwa amani na bila ya kutiwa aibu.

Ndiyo maana alipojitosa kwenye kura za maoni za kutaka kugombea tena ubunge, tena kwa ubishi licha ya kushauriwa mapema kuwa apumzike akaambulia kura kiduchu.

Katika mbio hizo mwaka huu, Dk. Mahanga alipata kura 2,381 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Scolastika Kivila, mama aliyepata kura 6,155 huku aliyeshinda akiwa ni Bonna Kaluwa ambaye aliibuka na kura 6,965.

Mbali na afisa huyo wa zamani wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kushindwa huko kwenye kura za maoni pia kulimkuta Msindai katika jimbo la Mkalama, mkoa wa Singida kwa kupata kura 3,908 huku mshindi akiwa ni Joseph Kiula aliyepata kura 5,223.

Kana kwamba haitoshi, Guninita mwenye umri wa miaka 56 alijitosa kugombea ubunge katika jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, lakini akaambulia kura 165 tu na kushika nafasi ya nane kati ya wagombea 10 huku mshindi, Abubakari Asenga (32) akipata kura 9,629.

Mbali na Dk. Mahanga, Msindai na Guninita, mwingine aliyetupwa katika kura za maoni na kukimbilia Chadema anakodhani ataupata ubunge ni Saidi Nkumba.  

Akiwa amejitosa ili kutetea nafasi hiyo kwa awamu nyingine, Nkumba alipata kura 3,236 tu huku akishindwa na George Kakunda aliyepata kura 4,109 katika jimbo la Sikonge, mkoa wa Tabora.  

Aidha, Modestus Kilufi aliyekuwa amejitosa ili kutetea nafasi hiyo aliyokuwa nayo katika jimbo la Mbarali, mkoa wa Mbeya alishindwa baada ya kupata kura 7,114 huku mgombea mpya wa kiti hicho kupitia CCM, Haroun Mulla akiibuka na kura 8,556 na kudai chama hicho kwamba “hakitendi haki”.

Mwingine katika orodha hiyo ni Lawrence Masha, mbunge wa zamani wa Nyamagana aliyewahi pia kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na mmoja kati ya wapambe wakubwa wa Lowassa.

Habari zilizothibitishwa na baadhi ya watu wa karibu ya Lowassa zinasema kwamba Masha, kama rafiki yake huyo angeteuliwa kugombea urais kupitia CCM na hatimaye akashinda angempa ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 10 za rais, kisha angemwingiza katika baraza lake la mawaziri.

Lakini alipokwama, Masha alijitosa kugombea ubunge huko Sengerema, hatua aliyochukua baada ya kugundua kuwa hakubaliki katika jimbo lake la Nyamagana ambalo lipo jijini Mwanza.

Licha ya kwenda Sengerema, Masha alishika nafasi ya nne akiambulia kura 3,254 tu huku mshindi wa mbio hizo katika jimbo hilo, William Ngeleja akizoa kura 15,845 na hicho ndicho kikasababisha akimbilie Chadema.

Aidha, Sioi Sumari ambaye pia alijaribu kugombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki kama alivyofanya mwaka 2012 naye alianguka tena.

Katika kura hizo za maoni za ndani ya CCM, kijana huyo ambaye ni mume wa binti mkubwa wa Lowassa alipata kura 4,038 huku John Sakaya akiibuka mshindi kwa kupata kura 12,729.

Kutokana na hali hiyo, Sioi aliamua kwenda Chadema kwa sababu ya uchu wake wa madaraka, na pia alifanya hivyo ili pengine asinyang’anywe mkewe ambaye ni mtoto wa Lowassa.

Naye kwa upande wake, Mgeja ambaye inabidi nitangaze kwanza maslahi kwamba ni mjomba wangu ilikuwa ikingojewa tu kuwa ni siku gani ataondoka ili kumfuata Lowassa.

Kati ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa yote iliyopo nchini, Mgeja alikuwa ndiye mpambe namba moja wa Lowassa akifuatiwa na Msindai, kisha anakuja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Onesmo ole Nangole na Guninita.

Mgeja na Msindai kwa mfano walikuwa sambamba na Lowassa katika kila kijiji, mtaa, kata, tarafa, wilaya mpaka mkoa alipokuwa akitafuta wadhamini wakati wa kuchukua na kuruudisha fomu za kuomba kugombea urais kupitia CCM kati ya Juni 3 na Julai 2, mwaka huu.

Wote kwa pamoja walikuwa wakifanya hivyo kinyume cha maelekezo ya CCM, lakini inawezekana ‘walilewa’ fedha za Lowassa na hivyo wakajisahau kuwa ni viongozi wanaopaswa kuwa mfano wa kuheshimu Katiba ya Chama chao, kanuni, taratibu na miongozo mingine na kubaki ‘wakimwabudu’ yeye.

Wanafahamu vizuri kuwa Lowassa anayetaka urais kwa nguvu zake zote anatumia mamilioni ya fedha ili kuisaka nafasi hiyo, lakini kinachofanywa ni propaganda za kipuuzi zinazolenga kuwadanganya wananchi ikiwemo kukodi bodaboda, kuzilipia mafuta ‘sheli’ huku magari na wasindikizaji wengine nao ‘wakijazwa’ kwa malipo maalum.

Sitaki nitoboe ukaribu uliopo kati ya Lowassa na mjomba wangu Mgeja ambaye ni binamu yake na marehemu mama yangu mzazi, lakini naye namuomba asiendelee kuwadanganya Watanzania ili kukidhi matakwa yake ya kisiasa ama kiuchumi.

Inawezekana hakifahamu kile ninakichojua kuhusu undani wake kwa Lowassa, lakini inaudhi zaidi anapokuja na uzushi, uongo na upotoshaji mkubwa unaolenga ‘kumchafua’ Rais Kikwete kwa sababu tu anataka aendelee kumnyonya rafiki yake huyo, yule ambaye Februari 6, 2008 alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kutajwa katika kashfa ya Richmond.

Sitaki pia niyaweke hadharani ninayoyafahamu kuhusu uongozi wake alipokuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga kwa sababu ni mjomba wangu, na pia ninafanya hivyo ili kumlindia heshima yake mwenyewe na hata Lowassa wake huyo, lakini nitashindwa endapo ataendelea kupotosha ukweli kwa makusudi.

Pamoja na kutotaka kumuumbua, lakini ninapenda nionyeshe angalau tu kidogo kuwa mjomba wangu huyo ni muongo linapokuja suala la maslahi yake.

Jumamosi iliyopita, Mgeja alinukuliwa na gazeti moja litolewalo kila siku nchini akikanusha ukweli wa kuwepo kwake Dodoma, siku tisa zilizopita ili kumpigania binti yake, Sinzo Mgeja apate ubunge wa Viti Maalum kupitia UVCCM.

“Mchakato huo ulikuwa ni wa kina mama. Nitawezaje kuingia kwenye mkutano huo? Labda mimi na Katibu (Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana tungebadilisha jinsia”, alisema kama alivyonukuliwa na gazeti hilo akimjibu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyesema kuwa alikuwepo Dodoma kwa ajili hiyo.

Pamoja na kukanusha hivyo na kutoa kejeli, Mgeja alikuwepo Dodoma akiwaomba akina mama wamchague binti yake huyo ili awe Mbunge wa Viti Maalum, lakini aliposhindwa akachukia na kutohudhuria kikao cha NEC kilichofanyika Jumatano na Alhamisi za wiki iliyopita, kisha akaibukia Chadema ilipofika kesho yake.

Katika mbio hizo za kutafuta uwakilishi wa wananchi bungeni, Halima Bulembo aliyeshika nafasi ya kwanza kati ya wagombea 26 alipata kura 109 huku Sinzo akiambulia kura 42.

Nafahamu kuwa Dk. Mahanga naye alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wa juu kabisa wa serikali waliokuwa ni wafuasi wakubwa wa Lowassa, lakini alikuwa akifanya hivyo kwa sababu aliamini kuwa ndiye rais wa tano wa nchi hii.

Sitaki pia kuyaweka wazi baadhi ya mambo yanayosemwa kuhusu naibu waziri huyo wa zamani, lakini tu ole wake naye iwapo ataanza kuwadanganya wananchi kama alivyofanya siku akitangaza kuwa anakwenda Chadema kumfuata Lowassa.

Kuhusu Msindai na Guninita, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Paul Makonda kwa mfano aliwahi kusema, na hapa ninanukuu:

“Yupo mtu anayewatumatuma hawa watu, amewafanya kuwa vibaraka (wake). Leo hii tutamjibu Msindai, Mwenyekiti (wa CCM wa Mkoa) wa Singida, kesho tutamjibu Guninita na keshokutwa tutamjibu nani (sijui) lakini nani aliyeko nyuma yao anayewatuma? Anaitwa Edward Ngoyai Lowassa...”

Sitaki kuwataja wote waliokwenda Chadema katika kipindi hiki cha mpito, lakini katika ujumla wao ama ni wapambe wa Lowassa mwenyewe ama ni wale walioshindwa kura za maoni za ndani ya CCM, hivyo walichofanya ni kutafuta kichaka ili kwenda kumalizia hasira au kuficha aibu kwa wake zao nyumbani, watoto wao na hata vinginevyo.

Mungu Ibariki Tanzania!


Napatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0787 088 870

WANAOKWENDA CHADEMA AMA NI WAPAMBE WA LOWASSA AMA WAMESHINDWA KURA ZA MAONI

Na Charles Charles SITAKI kumjadili mtu mwingine yeyote aliyekikimbia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Mae... [Read More]

Na Charles Charles
IPOKUWA katika ziara zake za kutafuta wadhamini 200 ili kukidhi matakwa ya kisheria, mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa aliahidi kuingilia mpaka uhuru wa mahakama nchini.

Akihutubia katika Uwanja wa Nzovwe mjini Mbeya, Ijumaa iliyopita, Lowassa alisema moja kati ya mambo atakayoyashughulikia kwa haraka kama atashinda uchaguzi mkuu ujao, ni pamoja na kumwachilia huru Babu Seya.

Mbali na Mbeya, mgombea huyo wa urais anayeungwa mkono na vyama vyote vinavyounda kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliirudia tena kauli yake hiyo siku moja baadaye alipokuwa katika jiji la Arusha.

"Tukiingia madarakani tutamwachia huru Babu Seya", alisema, kauli iliyoibua mshangao mkubwa miongoni mwa watu makini waliokuwa wakimsikiliza uwanjani, na pia ikashangaza wengi waliokuja kuisoma katika gazeti moja litolewalo kila siku nchini, kesho yake.

Nguza Viking, mwanamuziki mpiga solo, mwimbaji na mtunzi ambaye ni maarufu zaidi kama Babu Seya, anatumikia kifungo cha maisha jela katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam tokea mwaka 2004.

Alitiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Ilala katika jiji hilo, kisha akahukumiwa kutumikia adhabu hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya Mwaka 2001.

Hata hivyo, mawakili wake wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania wakipinga hukumu hiyo kwa madai kuwa hakutendewa haki.

Katika hatua hiyo, Mahakama Kuu iliyosikiliza rufaa hiyo iliitupilia mbali, hivyo adhabu dhidi yake ikaendelea kama ilivyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu.

Lakini pia, mawakili wa Babu Seya bado hawakuridhika, hivyo wakakata tena rufaa katika Mahakama ya Rufani Tanzania, kule ambako ilisikilizwa na jopo la majaji watatu kama sheria inavyoelekeza.

Hata hivyo, jopo hilo nalo liliridhia hukumu hiyo dhidi ya Nguza, lakini bado Marando akaonyesha nia ya kuendelea kumpigania mteja wake huyo.

Katika hatua hiyo, wakili huyo aliomba, kuwa Mahakama ya Rufani iteue jopo la majaji watano ili waipitie tena adhabu hiyo akiamini mteja wake huyo alizushiwa tuhuma hizo zote.

Ili kumpa haki yake, mahakama hiyo ilikubaliana na maombi ya Marando ya kuteua jopo hilo la majaji watano, wale ambao pia waliridhika pasipo na shaka kuwa hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Babu Seya ilikuwa ya haki.

Katika kesi ya msingi dhidi yake na wenae watatu, wawili kati yao wakifanikiwa kuachiliwa huru baadaye, Babu Seya alituhumiwa kubaka, kunajisi na kulawiti watoto wadogo, wale ambao kuna wengine walikuwa na wastani wa miaka 10 tu!

Miaka 11 baada ya hukumu hiyo kutolewa dhidi yake, mgombea urais anayetaka kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii anakuja na ahadi ya kumwachilia huru mhalifu huyo endapo atashinda uchaguzi mkuu ujao!

Siyo kazi yangu kumwandikia hotuba za kuzungumza anapokuwa mikutanoni, na pia si jukumu langu kumwelekeza cha kusema hususan kero au mahitaji ya Watanzania.

Pamoja na hayo na hata vinginevyo, Watanzania bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, dini zao, makabila yao, rangi za ngozi zao, kazi zao, maeneo yao, rika zao ama jinsia zao na kadhalika kamwe hawana hitaji la kutaka kuachiliwa kwa mhalifu yeyote.

Aidha, Watanzania nikiwemo mimi hawahitaji, kwa namna yoyote ile kuachiliwa kwa mhalifu wa aina ya Babu Seya aliyetiwa hatiani kwa makosa  ya ubakaji, kunajisi au kulawiti hadi watoto wa miaka 10 tu!

Tumeona maendeleo makubwa kabisa yaliyoletwa na serikali zilizopita hadi hii ya sasa, zote zikiongozwa kwa makini na viongozi waliotokana na Chama Cha Mapinduzi, kile ambacho wengi wanakijua kwa kifupi cha CCM.

Ilianza Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya uongozi thabiti wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ilifuatia Serikali ya Awamu ya Pili, nayo ikiongozwa na mwalimu kitaaluma, Alhaji Ali Hassan Mwinyi kuanzia Novemba 5, 1985 hadi Novemba 21, 1995.

Hiyo nayo ilifuatiwa na Serikali ya Awamu ya Tatu, safari hii ikiongozwa na mwandishi wa habari na mwanadiplomasia, Benjamin Mkapa aliyekuja kujulikana zaidi kama 'Mzee wa Ukweli na Uwazi'.

Huyo alipong'atuka Novemba 21, 2005 iliingia madarakani Serikali ya Awamu ya Nne, pia ikiongozwa na mwanadiplomasia mwingine na afisa mwandamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Jakaya Kikwete.

Katika mpangilio wake huo na chini ya viongozi hao kila moja kwa wakati na enzi zake, serikali zote hizo zilikuja na mikakati yake ya maendeleo kwa taifa na wananchi wake.

Sitaki kurejea nyuma hadi wakati wa utawala wa hayati Mwalimu Nyerere, Alhaji Mwinyi au Mkapa, lakini serikali ya sasa, chini ya Rais Kikwete nayo imefanya mambo mengi makubwa ya maendeleo.

Mfano ni pamoja na mikoa takribani yote nchini hivi sasa, kwa kiwango kikubwa kabisa kuunganishwa kwa barabara za lami.

Akizungumza katika hafla ya wizara yake ya kumuaga Rais Kikwete kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli alisema mtandao wa barabara za lami uliopo hivi sasa nchini ni kilomita 17,700  kutoka chini ya 6,000 zilizokuwepo mwaka 1995.

Mafanikio mengine ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari kwa kila kata, kupandishwa hadhi kwa hospitali zote za mikoa kuwa za rufaa, kuongezeka kwa vyuo vikuu ama vyuo vikuu vishiriki na hata kuwepo kila mkoa nchini na kadhalika.

Pamoja na kusahihisha kidogo kauli yake kuhusu Babu Seya alipokwenda Arusha, bila shaka baada ya kusutwa na viongozi wenzake, suala zima la mfungwa huyo, tena aliyetiwa hatiani kwa makosa ya ubakaji, ulawiti na kunajisi watoto wadogo kabisa kamwe siyo hitaji la Watanzania wa leo wala wa kesho.

Hata miye nisiyekuwa mwanasheria ninafahamu, kwamba makosa hayo kwa mhalifu aliyefungwa kwa kuyatenda kamwe hapewi msamaha wowote ukiwemo wa rais.

Kama siyo udhaifu wa kufikiri kama mgombea urais, nani kamdanganya Lowassa kuwa hitaji la Watanzania ni kuachiliwa huru Babu Seya?


Napatikana kwa Simu Na. 659 220 220 na 0787 088 870

HITAJI LA WATANZANIA NI KUACHIWA KWA BABU SEYA?

Na Charles Charles IPOKUWA katika ziara zake za kutafuta wadhamini 200 ili kukidhi matakwa ya kisheria, mgombea wa kiti cha Rais wa J... [Read More]

owassa aliyekuwa fisadi akiwa
CCM hata Chadema ni yuleyule

Na Charles Charles

JUMAPILI iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Meja Joseph Butiku aliwashangaa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kumkaribisha Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa, Edward Lowassa kuwa mwanachama wao.

Aidha, Butiku aliyewahi kuwa Katibu wa Rais kuanzia mwaka 1965 hadi 1985 wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliwashangaa zaidi kwa kumteua Lowassa kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza kwenye mdahalo kuhusu umuhimu wa maadili katika kuimarisha amani, haki na umoja kuelekea uchaguzi mkuu ujao, Butiku alisema Lowassa ni kiongozi mwenye tuhuma za siku nyingi za ufisadi.

Alisema Lowassa na wenzake kadhaa ambao hakuwataja kwa majina, wamekijengea Chama Cha Mapinduzi (CCM) mazingira ya 'kunuka' kutokana na hulka yao ya kutoridhika, uchu wa madaraka na kutaka kujitajirisha kwa njia 'chafu" kwa kutumia 'kichaka' cha siasa.

Katika hali hiyo, Butiku alisema Lowassa na wapambe wake walipaswa kutoka siku nyingi ndani ya CCM.

"Waondoke (na Chadema) wapokeeni tu. Kama hukubaliani na msimamo wa mwenye nyumba (akimaanisha Katiba, Kanuni na Taratibu za CCM) unatoka na siyo kuchafua nyumba ya watu", alisema.

Akionyesha kuwa anajua mambo mengi, Butiku ambaye ni Meja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alisema pia watu 'wamenunuliwa' , jambo ambalo limefanyika pia kwa vyombo vya habari ili vifanye kazi ya matajiri hao.

"Tunajua (kwamba) wengi wamenunuliwa na wanaonunua vyombo vya habari hawafai kupewa (uongozi wa) nchi.

"Wamewanunua (mpaka) vijana wa vyuo vikuu, wanamwaga fedha kwa vijana wa pikipiki (au bodaboda) hadi wanakanyagana, kuumizana na kudhalilika. Ni bora walivyoondoka CCM na hata hivyo walivumiliwa kwa muda mrefu".
Akirejea historia ya tuhuma za ufisadi dhidi ya Lowassa mwaka 1995, Butiku alifichua kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ndiye alimshtaki mbunge huyo wa zamani wa Monduli, Arusha kwa Baba wa Taifa kwamba ni fisadi asiyefaa kuwa rais wa nchi hii.

"Hivi mnajua kuwa aliyemshtaki Edward (Lowasaa kwa Mwalimu Nyerere) alikuwa Mwinyi, (wakati huo akiwa rais?)

"Unajua nchi hii bado changa sana. Mambo mengine unayaacha tu ili (Tanzania) isivurugike. Lakini ukiamua kuyasema mambo ya Edward (yanatisha) na mimi nayajua", alibainisha.

Naam! Hayo siyo maneno yangu ila yanatoka kinywani mwa Butiku, Katibu wa Rais na Mkuu wa Mkoa Mstaafu aliyeanza kazi wakati Lowassa akiwa mtoto wa chekechea.

Anaijua Tanzania na misingi yake kama anavyokijua chumba anacholala nyumbani kwake. Anawajua watu wengi walioanza kazi wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, mmoja kati yao akiwa ni Edward Lowassa.

Anaijua vizuri CCM na sababu za kuundwa kwake kuliko Lowassa aliyekuja baadaye, tena akitokea chuoni kuja kufanya kazi akiwa hajui lolote wala chochote.

Namshukuru afande wangu Butiku kwa kusema yale ambayo, kwa namna yoyote ile kama ningeyasema miye wapambe wake wakiwemo ninaowajua vyema, wengine ni waandishi wa habari wakongwe wangenimwagia kila aina ya uzushi na matusi.

Nampongeza kwa kuwa amejitosa waziwazi kusema ukweli anaoujua, ule ambao kwa wengine utakuwa wa shubiri.

Sina sababu ya kuendelea kurejea kile kilichozungumzwa na Butiku, lakini hotuba yake angalau imeweza kuwafumbua macho baadhi ya wapambe wakubwa wa Lowassa, wale ambao kuna wengine wanatumika kama dodoki bila wao kufahamu.

Nimekuwa nikiandika mara kadhaa kuhusu uovu wa kutafuta urais unaofanywa na Lowassa, wapambe wake ama sasa na viongozi wa Chadema yenyewe.

Ingawa Butiku mwenyewe hakutaja gazeti, kituo cha redio au televisheni wala mwandishi wa habari 'aliyenunuliwa', ukweli kuhusu jambo hilo unajionyesha hata kwa taahira wa akili.

Ijumaa iliyopita kwa mfano, waandishi wa habari na watangazaji wa baadhi ya vyombo vya habari nchini, walikodiwa ndege maalum na Lowassa au kwa uwezeshaji wake kutoka Dar es Salaam hadi Mbeya ili wakaandike vizuri habari zake za kutafuta wadhamini.

Kutoka huko walipelekwa hadi Arusha, Mwanza na hatimaye visiwani Zanzibar utadhani ni watumishi wake mwenyewe.

Walipelekwa kwa usafiri huo wa gharama kubwa zaidi kuliko wote duniani, lakini pili walilipwa pia posho na huenda walikuwa wakilipiwa hadi malazi yao, chakula na hata vinginevyo.

Inawezekana walifanyiwa hayo yote kwa sababu, kikubwa anachohitaji Lowassa ni kuzuia baya lake lolote lisiandikwe wala kutangazwa na chombo chochote kile cha habari.

Wale wanaofahamu kuhusu suala hili watakuwa na kumbukumbu nzuri, kwamba hata wakati akitafuta wadhamini kwa ajili ya kuomba uteuzi wa kugombea urais kupitia CCM, Lowassa alikuwa 'akimiliki' na kuzunguka na timu maalum ya waandishi wa habari.

Alikuwa akizunguka nao kwa magari ya kifahari aina ya Landcruiser VX, na pia alikuwa akipaa nao kwa ndege kama ilivyokuwa kutoka Iringa hadi Songea, mkoa wa Ruvuma.

Mtu anayekuchukua kutoka Dar es Salaam na kuruka naye kwa ndege hadi Mwanza, ukasafiri kwa magari ya kifahari kutoka huko hadi Geita, Mara, Simiyu, Geita, Shinyanga, Tabora na kadhalika kwa gharama zake yeye hakika huwezi kuandika maovu yake ila kumpamba hata kwa uongo.

Haiwezekani akuzungushe kila mkoa huku akikulipia mahitaji yako yote kama mwanaye, anakulipa mpaka posho ya shilingi 100,000 kila asubuhi na kukukirimu kwa kila kitu halafu uandike maovu yake.

Kama mwandishi wa habari anafanyiwa hayo yote, halafu anayemkirimu anazunguka naye muda wote inabidi awe na roho ngumu kama ya paka ndipo aweze kuandika ukweli.

Ndiyo maana wakati wote wa kutafuta wadhamini ndani ya  CCM, waandishi wa habari aliokuwa akizunguka nao hata siku moja hawakuandika maovu yake.

Walishindwa kuhabarisha kwa mfano namna watu, katika baadhi ya maeneo walivyokuwa wakigombea au kuhoji posho walizokuwa wakiahidiwa ili kwenda kumdhamini.

Hakuna aliyeweza kuandika ama kutangaza jinsi walivyokuwa wakisombwa na malori, tena ya kukodi wakitolewa takribani kila eneo la mkoa anaokwenda.

Mfano mmojawapo ni Mbeya ambako watu walisombwa namna hiyo kutoka wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Mbarali, Kyela, Rungwe, Ileje, Momba, Mbozi, Chunya na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Wapo waliotoka hadi nje ya Mbeya kwa kusafirishwa kutoka Rukwa, Njombe na Iringa huku alipokwenda Mwanza wakitolewa mpaka Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Kagera, Geita, Mara, Manyara, Arusha na wengine Kilimanjaro.

Pamoja na kusaka 'mafuriko' hayo ya 'kutengeneza', watu wamekuwa wakidanganywa vinginevyo ili 'kumbeba' tajiri huyo kwa gharama zake.

Kama alivyobainisha Butiku, harakati za Lowassa za kutaka kwenda Ikulu kwa gharama zozote zimewakumba hadi wanafunzi wa vyuo vikuu, waendesha bodaboda na makundi mengine kwa kuwalipa mamilioni ya fedha.

Pamoja na 'uchafu' wote huo  kujulikana hadharani, vyombo kadhaa vya habari kamwe haviandiki au kutangaza chochote.

Ndiyo maana haishangazi kusikia kuwa baadhi ya wahariri wa magazeti, vituo vya redio na televisheni nchini wiki kadhaa zilizopita wamelipwa shilingi 1,000,000 kila mmoja.

Tunaambiwa fedha hizo wamelipwa ili wazuie taarifa zote za udanganyifu wa Chadema au Lowassa, na pia wahakikishe chama hicho na mgombea wake huyo wa urais wanapambwa kwa namna zote.

Mimi mwenyewe ni shahidi wa posho hizo za Lowassa kwa waandishi wa habari.

Niliitwa na kaka yangu huyo mwaka 2011 kwenda ofisini kwake, Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako aliniambia, na hapa ninanukuu:

"Wewe ni mwandishi mzuri wa makala. Naomba unisaidie kunipamba kwenye magazeti ambapo, kila mwezi utakuwa unakuja hapa unachukua shilingi 300,000", aliniambia Lowassa kwa kinywa chake mwenyewe na kuongeza:

"Usiponikuta mimi utakuwa unamkuta sekretari wangu na atakupa, nitamwelekeza".

Kwa vile isingewezekana ofisini kwake kumwambia "hapana", kauli yangu kwake ilikuwa ya maneno manne tu: "Hakuna tatizo Mheshimiwa, nitafanya".

Nilipomwambia hivyo, Lowassa aliinama chini ambapo, kiasi cha dakika moja hivi baadaye aliinua macho yake na kunikabidhi shilingi 300,000 taslimu kama mfano, zote zikiwa noti za shilingi 10,000 kila moja.

Nilimpa mkono na kumwambia "nashukuru sana", lakini baada ya kumuuga na kuondoka sikurudi tena, na pia sikuwahi kuifanya kazi hiyo hadi leo.

Sikutaka kufanya hivyo kwa jeuri moja tu ambayo pia nimekuwa nikiisema mara nyingi.

Siwezi 'kununuliwa' na mtu kwa fedha zake ili nimuunge mkono, nimpambe magazetini au niwe 'mtumwa' wake kwa namna moja ama nyingine.

Naweza tu kumuunga mkono mtu yeyote kwa kuangalia hoja zake, sifa zake na uwezo wake wa kazi anayoomba kuifanya na siyo vinginevyo.

Ndiyo maana sikushangaa nilipopata habari kuwa baadhi ya wahariri wa magazeti, vituo vya redio na televisheni nchini wamehongwa shilingi 1,000,000 kila mmoja ili wampambe Lowassa katika harakati zake za kutaka awe Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Ndiyo maana sikushangaa kusikia Butiku naye amekemea jambo hili.
Katika hali hiyo na hata vinginevyo, wale wanaodhani kuwa Lowassa aliyeitwa fisadi alipokuwa CCM, tena kwa kiwango kikubwa zaidi na viongozi wa Chadema yenyewe atabadilika kwa kwenda katika chama chao.

Daima atabaki yuleyule na vilevile kama zamani hata iweje.
Mtu akizoea kula nyama ya nguruwe hawezi akaacha eti kwa sababu tu amehamia kijiji kingine!

Napatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244

LOWASSA WA CCM NI YULE YULE WA CHADEMA

owassa aliyekuwa fisadi akiwa CCM hata Chadema ni yuleyule Na Charles Charles JUMAPILI iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasi... [Read More]

MAGUFULI AJITAMBULISHA ZANZIBAR

[Read More]



Na Charles Charles

IJUMAA iliyopita, wabunge wote wa kambi ya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliokuwa kwenye kikao cha nne cha mkutano unaoendelea sasa mjini Dodoma, walitoka nje ya ukumbi na kwenda kuongea na waandishi wa habari kwa dakika 38.

“Tumewaita kuzungumzia sababu za kutoka nje na hatua za kuchukua. Kama mlivyosikia, (James) Mbatia (ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa anayetoka NCCR – Mageuzi) alisema hakuna mitaala na (wala) haijawahi kuwepo tangu mwaka 1961 na kama ipo atajiuzulu”, alisema aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho na Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

Alidai kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema uongo bungeni kwamba wizara yake ina mitaala ya masomo kwa shule za sekondari na msingi, lakini akashindwa kuitoa.

“…Tutapeleka taarifa ya kikao chetu katika Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kumtaka Waziri Kawambwa ajiuzulu kwa kulidanganya bunge, ikishindikana tutaipeleka tena katika mamlaka zilizomteua”, alibainisha.

Aliongeza kuwa endapo mamlaka hiyo pia haitamwajibisha, wabunge hao watapiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili kuilazimisha serikali nzima ijiuzulu, hatua itakayomfanya Rais Jakaya Kikwete ateue baraza jipya la mawaziri kama ilivyokuwa Februari 6, 2008 wakati aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Edward Lowassa alipoamua kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa.

Mbali na kufanya hivyo dhidi ya Pinda, wabunge hao waliwaambia waandishi wa habari kwamba wataandaa hoja nyingine ya kuwang’oa Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai kwa tuhuma za kukandamiza hoja zao.

“Tulitaka kujadili hoja ya gesi ya Mtwara, lakini Spika akaizima, akasema itaundwa tume, baadaye tume hakuna baada ya Waziri Mkuu kwenda (huko). Tangu Mbatia awasilishe pia hoja yake inaonyesha waziwazi (kwamba nayo) wanataka kuizima”, alisema Tundu Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani katika bunge hilo la 10.

Nasema siyo lazima mtu awe mpaka mwanasheria, daktari wa falsafa au profesa wa fani yoyote ndipo aweze kuuona ujinga unaofanywa na kambi hiyo ya upinzani isipokuwa hata akisoma kwa kawaida.

Haiwezekani kwamba serikali bado haina mitaala ya elimu nchini tangu nchi yetu ipate Uhuru wake mwaka 1961 hadi leo, madai ambayo ni uongo uliovuka mpaka na kuwa ni uzandiki unaotia ukakasi hata kuuzungumza mdomoni.

Ingawa ni kweli kuwa mimi siyo mwalimu na kamwe sikusudii kufanya kazi hiyo hata siku moja hapo baadaye, lakini najua mitaala ya masomo kwa shule za msingi na sekondari hapa nchini ipo, hivyo anayesema vinginevyo ingekuwa bora kama angetuambia kwamba anayodai yeye imechelewa kuanza na kueleza imechapishwa lini ili umma ufahamu. 

Nilipokuwa nasoma mwaka ule wa mwisho wa elimu yangu ya msingi nilichukuliwa na mjomba wangu aliyekuwa mwalimu mkuu shuleni kwetu, hivyo nilikuwa naziona nakala za mitaala hiyo ambayo haikuwa ya mwaka 1960, 1959 au 1958 ya kabla ya Uhuru kwa sababu hata marehemu mama yangu mzazi alikuwa bado ni mtoto wa miaka 11 tu wakati Tanzania Bara inajitawala hapo Desemba 9, 1961.

Nilikuwa naishi palepale shuleni na mjomba wangu huyo na baadhi ya walimu, hivyo nilikuwa pia naona wakiandaa masomo ya kwenda kutufundisha madarasani siyo kwa matakwa yao wenyewe, bali walitumia mitaala hiyo ya elimu inayotungwa serikalini. 

Mbatia aliyeshindwa kukijenga chama chake ambacho yeye ndiye Mwenyekiti wa Taifa anadhani atakijenga kwa kuwasilisha hoja hizo za uongo na uzushi bungeni. 

Anadhani kwa kufanya hivyo kitafufuka tena kama ilivyokuwa Februari 28, 1995, siku ambayo aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Augustine Lyatonga Mrema alipohamia huko akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na uchu wake wa kutaka kugombea urais.

Anadhani kitafufuka na kuwa na nguvu kiliyodumu nayo kuanzia hapo hadi mchana wa Jumapili Aprili 25, 1999, siku ambayo Mrema alitangaza ghafla tena kuachana na chama hicho na kuhamia Tanzania Labour Party (TLP) na kusambaratika nchi nzima siku ileile.

Endapo anatumia hoja hiyo akidhani itamjenga kisiasa au chama chake basi aelewe kuwa amedanganywa kama mtoto anayesoma shule ya chekechea. Ni vizuri akimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kumteua kushika nafasi hiyo, ile ambayo alijitosa kuigombea mwaka 2010 katika jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam na kushindwa vibaya.

Anapaswa ajue kwamba hakuteuliwe ili akafanye utapeli wa kisiasa bungeni, ule ambao ni pamoja na kudai Tanzania haijawahi kuwa na mitaala katika shule za msingi na sekondari tangu ipate Uhuru wake mwaka 1961!

Aliteuliwe kuwa mbunge ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 66(e) na 67(a) na (c) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa. 

Hakuteuliwa kwenda kutumia nafasi hiyo ili kusema uongo, uzushi, umbeya wala kufanya uchochezi wowote au uchonganishi kati ya Watanzania na serikali ya nchi yao. 

Haiwezekani kwamba eti Waziri wa Elimu awe anazunguka na mzigo wa nakala za mitaala ya shule kila anakokwenda iwe bungeni, ndani ya vikao vya kiserikali ama pale anaposafiri kikazi nje ya nchi ili kama atatakiwa kuzungumzia suala hilo anazionyesha papo kwa papo.

Kama alivyosema hata Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, serikali katika kikao kilichopita iliahidi kuwasilisha mitaala hiyo katika kikao hiki cha sasa na kuhoji: “Sasa wasiwasi wa mbunge (Mbatia) ni nini? Tutaileta hata siku ya mwisho ya bunge”.

Tayari serikali imewasilishwa bungeni jana, Jumatano ambapo kila mbunge anatakiwa kupata nakala yake mwenyewe.

Sipendi kuamini kuwa Mbatia, Tundu Lissu, Mrema na wabunge wengine wote waliotoka nje ya bunge, Ijumaa iliyopita ni kama watoto wa chekechea katika kuchanganua mambo. Sitaki kabisa niamini kwamba akili yao bado nyembamba wakati wote wana umri wa zaidi ya miaka 18. 

Mchukulie Mrema kwa mfano ambaye kama asingekimbilia bungeni angekuwa tayari ni mtumishi mstaafu wa umma kwa vile miaka yake duniani iko kwenye 70. Leo naye eti anaunga mkono upuuzi wa vijana kama Mbatia aliyezaliwa mwaka 1964 na Tundu Lissu aliyezaliwa mwaka 1968!

Kuhusu hoja ile ya kutaka Waziri Kawambwa ajiuzulu na asipofanya hivyo watapiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda nasema lengo hilo pia ni ulevi wa madaraka waliyopewa ya uwakilishi wa wananchi bungeni.

Wandhani kuwa kwao ni wabunge basi wana akili kuliko wananchi wengine. Wanafikiri wanajua mambo mengi zaidi kuliko wote wasiokuwa wabunge, ujinga ambao mtu yeyote akiamini hivyo huwa ni mwenzawazimu kichwani.

Nakubaliana kwa asilimia 100 kuwa bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kama inavyobainishwa katika Ibara ya 53A(1) ya Katiba ya nchi inayosema:

“Bila kuathiri masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii, bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja (ya) kupendekeza hivyo na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii”.

Hata hivyo, Ibara ya 53A(2) ya Katiba ileile inasema bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hiyo, hoja yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bado haiwezi kutolewa endapo ina mapungufu yafuatayo:

(a) Haina uhusiano wowote na utekelezaji wa majukumu ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 52 ya Katiba, na pia kama hakuna madai kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) Haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo;

(c) Haijapita miezi tisa tangu hoja hiyo pia itolewe bungeni na kukwama kupitishwa na wabunge walio wengi.

Kana kwamba haitoshi, Ibara ya 53A(3) inasema hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bado haiwezi kupitishwa bungeni isipokuwa kama itakidhi mambo yafuatayo:

(a) Itatolewa taarifa ya maandishi kwa Spika iliyotiwa saini na kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wote, lakini isipungue angalau siku 14 kabla ya siku iliyokusudiwa kuwasilishwa bungeni;

(b)  Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo bungeni yote yametimizwa.

Pamoja na hayo, Ibara ya 53A(4) inasema hoja iliyotimiza masharti hayo itawasilishwa bungeni mapema iwezekanavyo na halafu mwisho; kifungu kidogo cha tano kinaeleza: “Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu iwapo inaungwa mkono na wabunge walio wengi” (mwisho wa kunukuu).

Naomba ieleweke kuwa sisemi genge hilo la kina Tundu Lissu, James Mbatia, Augustine Mrema na wenzao haliwezi kujaribu kukidhi matakwa ya Ibara ya 53A(3)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliyoitaja. 

Najua litahangaika kutaka kufanya hivyo ili kusaka umaarufu kwa Watanzania wasiojua lolote wala chochote. Litajaribu kuwarubuni wale wasiojua ukweli likitaka wadanganyike kuwa linapigania haki zao, lakini linachotafuta hasa ni sifa tu za uongo, uzushi na malengo ya siasa za kitapeli.

Haiwezekani kwamba serikali iwe inahangaikia kujibu uzushi unaotengenezwa na kikundi cha wabunge wachache wenye uchu wao wa madaraka, wale ambao wametumwa kwenda kuwasemea wananchi bungeni kwa masuala ya kweli na siyo kutunga umbeya na uzandiki.

Hakuna mpiga kura aliyewatuma kwenda kumng’oa Waziri Mkuu au kushinikiza Waziri wa Elimu kuwa lazima ajiuzulu. Waliapa kuwatumikia Watanzania wote kwa uaminifu ambao ni pamoja na Mizengo Pinda, Dk. Kawambwa na wengineo na kamwe hakuna hata mmoja aliyeagiza kwamba wakifika bungeni kazi yao kubwa iwe ni kutoka nje ya vikao. 

Hakuna mwananchi aliyewatuma wakalazimishe kuwa hoja zao hata kama za uongo na uzushi ni lazima zitekelezwe kwa jinsi wanavyotaka wao, na kwamba zikipingwa ama kutolewa majibu na serikali basi iwe ni nongwa na kususia kama watoto wenye gubu kwa mama wa kambo.

Shinikizo la kutaka kuwang’oa mawaziri fulani kila wanapokwenda bungeni ni siasa zilizotengenezwa kwa chuki na wivu. Haiwezekani nchi yetu iwe na utamaduni kwamba kila kikao cha bunge akang’olewe waziri mmoja, wawili, watatu ama vinginevyo na pale inaposhindikana basi anatishiwa Waziri Mkuu.

Katika kikao kile cha Aprili, 2012, wabunge hao wa upinzani walijiorodhesha majina wakiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe wakitaka eti Waziri Mkuu Pinda ang’oke madarakani. 

Walifanya hivyo wakishinikiza kuondolewa kwa mawaziri sita ambao kwanza; Kamati ya Wabunge Wote wa CCM ilishauri kuwa wawajibishwe kisiasa siyo kwa sababu walifanya kosa lolote, jambo ambalo halina tatizo katika uongozi na utendaji serikalini.

Alipopata taarifa hizo kutoka kwa rafiki zake ambao ni baadhi ya wabunge wa CCM, Zitto alitaka palepale kuwa mawaziri hao wang’olewe “mara moja” utadhani wahalifu wa jinai. Akasema wasipotoka basi wapinzani wangepiga kura ya kukosa imani na Waziri Mkuu na hivyo yeye ndiye abebe msalaba wao.

Licha ya kuanza kujiorodhesha majina kwa mbunge huyo mwenyewe kukimbilia alfajiri katika lango la wabunge kuingia ukumbini ili kuwataka watie saini azimio hilo la hila, kanuni za bunge zilisababisha mpango huo mzima uyeyuke papo hapo utadhani tonge la siagi lililotumbukizwa motoni.

Akitekeleza ushauri wa busara wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko katika baraza hilo ilipofika Mei 7, 2012. Aliwapumzisha baadhi ya mawaziri huku wengine wakibadilishwa wizara na hata vinginevyo na hivyo kuzima hoja hiyo kwa hekima.

Lakini ilipopita miezi miwili tena baadaye, wabunge hao wa upinzani pamoja na wachache wa CCM wanaokuwa na chuki zao wenyewe wakaibuka na jambo jingine. Sasa wakataka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliackim Maswi eti wafukuzwe.

Muhongo aliyekuwa ndiyo kwanza amemaliza mwezi mmoja tu katika wizara hiyo akiwa na wadhifa huo alijengewa tuhuma za majungu, wivu, hasira na chuki za maslahi ya kisiasa na hata kiuchumi na kuanza kushinikizwa aondoke.

Naishukuru serikali hasa Rais Kikwete kwa kusema “hatoki mtu yeyote”. Aligoma kwa namna zote kuwang’oa madarakani au kuwahamishia mahali pengine. Namshukuru kwa kutosikiliza majungu yaliyotengenezwa na wabunge hao wenye chuki zao kwa CCM na serikali yake.

Mbali na kutaka Dk. Kawambwa ang’olewe katika mpango huo wa sasa, wabunge hao pia wanapanga kuwang’oa Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kwa tuhuma za kusitisha hoja ya kutaka suala zima la gesi iliyoibua vurugu kubwa kule Mtwara kuwa lijadiliwe bungeni. 

Baada ya awali Spika kusema kuwa angeunda Tume ya Bunge ili kwenda katika mkoa huo kupata ukweli, lakini alitangaza tena baadaye kwamba asingefanya hivyo kwa vile tayari Waziri Mkuu alikuwa amelishughulikia jambo hilo kwa namna zote na kupata suluhu yake.

Mbali na hayo, nani asiyejua ukweli kuwa wao ndio waliongoza uchochezi wote wa gesi ili kukidhi matakwa yao ya kutaka Tanzania isitawalike mwaka 2013? Nani hakumsikia kwa namna moja ama nyingine Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliposema kazi hiyo imefanywa na chama chake, na kwamba itaendelea mpaka mwaka 2015?

Leo wanapong’ang’ania iundwe tume ya uchunguzi pamoja na kutaka kulijadili suala hilo bungeni wanadhani kuwa nani hajui lolote wala chochote? Kwa nini serikali ipoteze fedha kwa kuwalipa wabunge waliotarajiwa kuwemo katika kikundi hicho wakati tayari undani na ukweli wa vurugu hizo zote umeshapatikana?

Mgogoro wa Mtwara uliratibiwa na wapinzani haohao kutoka vyama vinane vya siasa ambavyo ni pamoja na NCCR – Mageuzi ya Mbatia, TLP ya Mrema na pia Chadema ya Tundu Lissu, halafu hivi leo wanajidai kule bungeni kwamba iundwe tume ya kuchunguza uchochezi wao utadhani hawahusiki.

Walifanya hivyo kwa kutaka mwakilishi wao ndani ya tume hiyo ambaye ilikuwa lazima awemo, akakutane na viongozi wa umoja wa vyama vyao waliokuwa wakiratibu moja kwa moja uchochezi wao katika mkoa huo, kisha akisharudi Dodoma aje awape mrejesho. 

Walitaka awemo ili akakutane na Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama hivyo wilayani Mtwara, Uledi Abdallah pamoja na Katibu wake, Saidi Kulaga na hivyo kupata undani na ukweli wa sakata lote ili ikiwezekana walitengenezee uongo mpya ama pengine wahamie mkoa mwingine.

Nahitimisha kwa kuuliza swali moja kuwa je; hivi wabunge hawa wenye kazi kubwa ya kuchochea uasi kwa serikali, kupotosha ukweli na kususia vikao vya bunge wana faida gani kwa taifa kama siyo laana?

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244

Wabunge hawa wenye kazi ya kuchochea uasi na kususia vikao vya bunge ni laana

  Na Charles Charles IJUMAA iliyopita, wabunge wote wa kambi ya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioku... [Read More]

Lema anapiga marufuku 
wananchi kupata habari?

o Heche naye aonyesha anavyotumiwa na Dk. Slaa

Na Charles Charles

MBUNGE wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema amewalisha kiapo wafuasi wake cha kuwapiga marufuku kununua baadhi ya magazeti, kutazama vituo viwili vya televisheni na kutosikiliza kituo kimoja cha redio nchini.

Lema aliyekuwa akiwahutubia wafuasi wake hao kwenye Uwanja wa Kituo cha Mabasi cha Nduruma mjini humo, Jumamosi iliyopita, alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu, kabla ya kurudishiwa na Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam, siku moja kabla ya hapo. 

Katika hotuba yake hiyo, Lema aliwaambia wananchi waliokuwepo katika mkutano wake huo kwamba wasinunue magazeti ya UHURU, HABARI LEO, TAZAMA TANZANIA na JAMBO LEO, na kwamba wasiangalie kwa namna yoyote ile vipindi vinavyorushwa na Kituo cha Televisheni cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) pamoja na Star TV wala kusikiliza kituo cha Radio Five ya jijini Arusha.

Alisema kuwa magazeti hayo sambamba na vituo hivyo vitatu katika ujumla wake vimekuwa vikiisakama sana kihabari Chadema, jambo alilodai kwamba haviitakii mema isipokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na adhabu yake iwe ni kususiwa kununuliwa, kuangaliwa na hata kusikilizwa kwa namna zote.

Sikutarajia kuwa mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na hasa kinachodai siku zote kwamba kinapigania uhuru wa habari, uhuru wa mtu kushirikiana na watu wengine, uhuru wa kutoa maoni, haki ya kupata ujira wa haki pamoja na haki ya kumiliki mali ndiye anakuwa wa kwanza kuwanyima haki hizo zote wapiga kura wake. 

Ibara ya 18(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayoendelea kutumika sasa inaeleza ifuatavyo:

“Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii” (mwisho wa kunukuu).

Akiwa Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Lema alipaswa kuwa mstari wa mbele kwa juhudi na maarifa yake yote, kuhakikisha kwamba ibara hiyo ya Katiba ya nchi inaheshimiwa na kila Mtanzania, lakini inashangaza kuona badala ya kuitetea kwa nguvu zake zote, yeye ndiye anakuwa wa kwanza kuikiuka kwa kuwataka watu wavibague baadhi ya magazeti, redio na televisheni nchini ili wakose habari.

Ni ajabu kuona mbunge anakuwa na kinyongo na baadhi ya vyombo hivyo vya habari eti kwa sababu tu haviimbi utukufu wake kama vinavyofanya vile ‘vinavyomilikiwa’ kwa namna moja ama nyingine na chama chake, jambo ambalo ni ujinga kuvilazimisha vyote viwe kama midomo yake au kumsifu kila kwa kila neno analosema kinywani mwake hata kama halina faida yoyote kwa watu wengine, taifa letu, Afrika yetu au hata ulimwengu.

Ni ujinga kutaka eti magazeti yote, redio pamoja na vituo vyote vya televisheni nchini kila moja iwe inatangaza mambo anayoyataka mwenyewe au kuwaponda wengine, na kwamba kila anapowatukana wanachama, viongozi na wafuasi wa chama kilichopo madarakani ama serikali yake basi vyote vimuunge mkono katika hali anayoitaka yeye.

Bila ya kujali itikadi yake ya kisiasa na kuiona kuwa ni bora kuliko zote zilizobaki, Lema anapaswa aheshimu ukweli kwamba kila mtu ana haki ya kuwa na maoni na kueleza fikra zake kwa watu wengine, jambo ambalo linaelezwa vizuri katika Ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anapaswa akubali na kuheshimu ukweli kwamba kila mtu ana haki ya kuamini chama cha siasa anachokitaka yeye mwenyewe, ile ambayo imeelezwa katika Ibara ya 3(1) ya Katiba hiyo ya nchi inayosema ifuatavyo:

“Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, (na) yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa” (mwisho wa kunukuu).

Katika hali hiyo na hata vinginevyo, hatua iliyofanywa na Lema ya kuwalisha yamini wafuasi wake kuwa wasinunue magazeti ya UHURU, HABARI LEO, TAZAMA TANZANIA na JAMBO LEO, kutosikiliza kituo cha Radio Five wala kutoangalia Star TV na TBC1 ni ujinga uliovuka mpaka akilini.

Yeye mwenyewe anafahamu yamini yake kwa wafuasi wake siyo lolote wala chochote na hakuna yeyote anayeweza kuwa vyovyote pindi akienda kinyume chake.

Haiwezi kumdhuru yeyote hata iweje kwa sababu siyo Mungu wala taasisi ya kisheria. Ana mfano hai kuwa hata yamini aliyokula Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kwa Mungu wake siku alipotunukiwa ushemasi na upadri alikuja kwenda kinyume chake, lakini bado hakufanywa chochote.

Alimwahidi Mungu kwamba angeishi kiseja katika maisha yake yote, lakini akashindwa na kufunga ndoa na mwanamke wakati akiwa Mtawa wa Kanisa Katoliki, yule aliyepata naye watoto wawili na hatimaye akawatelekeza mkoani Manyara. 

Wote waliokula kiapo hicho mkutanoni siku hiyo kwamba hawatanunua kabisa magazeti hayo, hawataangalia vituo hivyo viwili vya televisheni wala kusikiliza kituo hicho cha redio hakuna hata mmoja ambaye kweli ataacha kwa kumhofia Lema isipokuwa kama pia ni mjinga wa kufikiri kichwani.

Pamoja na sababu nyingine, wengi waliapa kwa kuogopa macho ya watu ili kuepuka vipigo vya baadhi ya wafuasi wake ambao kuna wengine ni wendawazaimu vichwani kama yeye mwenyewe, lakini walipofika majumbani wakaendelea kuzingalia TV zote hizo zikiwemo taarifa zake za habari, na pia kuna wengine waliendelea kusikiliza Radio Five na kusoma magazeti yote hayo kwa namna moja ama nyingine.

Mbali na kuzuia uhuru wa kupewa taarifa za matukio ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli nyingine za watu, kiapo kilichotolewa na Lema kwa wafuasi wake pia kililenga kuzuia ajira kwa baadhi ya vijana wanaoishi, kutunza familia na kutoa huduma mbalimbali kwa wategemezi wao kwa kufanya biashara ya kuuza magazeti hayo bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.

Hatua yoyote ya kuwalisha watu kiapo kwamba wasiyasome maana yake ni kutaka vijana hao washindwe kuwahudumia wake zao, waume zao, watoto wao, baba zao, mama zao, babu zao, bibi zao, watumishi wao wa ndani na hata kutoa msaada wowote kwa ndugu zao wengine na kadhalika.

Anataka wakose ajira ili pengine wawe wezi wa mifukoni, vibaka wa usiku, matapeli wa mjini, majambazi wanaoua watu, makahaba wanaouza miili yao kwa kutoa mapenzi ya kawaida au kinyume cha maumbile yao na kufanya uhalifu mwingine.

Badala ya kuzungumzia ujinga na kuwalisha watu viapo vya kiwendawazimu mkutanoni, Lema alipaswa angalau ajibu tuhuma za jinai zinazoelekezwa kwake hivi sasa na baadhi ya vyombo vya habari zikiwemo za wizi wa kuaminika, ufisadi wa mali na misaada ya fedha na mali nyingine kwa chama chake na kutokuwa mwaminifu akiwa kiongozi mwandamizi wa Chadema na mbunge wa kuchaguliwa jimboni.

Likiandika katika toleo lake namba 220 la Jumanne Desemba 11 – 17, 2012, gazeti la FAHAMU litolewalo mara moja kila wiki lilidai kwamba Lema anatuhumiwa kutafuna fedha zilizochangwa na wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema ili kugharamia maandamano na mikutano ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) hata kama inafanyika kwa vurugu, fujo na umwagaji wa damu. 

Alipaswa aitumie nafasi hiyo kuwaambia wapiga kura wake endapo anahusika au hahusiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma za ‘kuingia mitini’ na pikipiki aina ya Kawasaki iliyotolewa msaada na wafadhili wa Chadema.

Alipaswa aseme ni wapi alikolipeleka trekta alilokabidhiwa na wafadhili wa Chadema ili kuwasaidia wajane kwenye mashamba yao, pembejeo ya kilimo aliyopewa pindi tu baada ya kuapishwa kwake na kuwa mbunge mpya wa Arusha Mjini mwaka 2010.

Alipaswa awaambie ni wapi lilikokwenda na ilikuwaje, hatua ambayo ingewezesha wajue endapo linafanya kazi aliyoelekezwa na wafadhili waliompa kwa ajili ya wajane hao, kina mama ambao kuna wengine waliachiwa watoto ama pengine wajukuu baada ya kufiwa na wapendwa wao.

Alipaswa awaeleze kuhusu ukweli wa tuhuma dhidi yake kwamba amekuwa akichangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wajane na watoto waliofiwa na wazazi wao na kuzitafuna zote, na kwamba anatumia propaganda zinazolenga kuwadhoofisha baadhi ya wanachama na viongozi wenzake wa Chadema.

Alipaswa ajibu tuhuma kwamba amekuwa akichangisha mamilioni ya fedha kutoka kwa matajiri wa Arusha akidai kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Taifa wa M4C, na kwamba hata fedha zilizochangiwa familia za marehemu waliopigwa risasi siku ya maandamano ya vurugu za Chadema za Januari 5, 2011 hadi sasa hazijawafikia walengwa.

Alipaswa azungumzie tuhuma kwamba amekuwa akikusanya fedha nyingi anazodai kuwa za kusomeshea watoto kupitia Shirika la Arusha Development Fund (ARDF), lakini zote au nyingi kati yake hazifahamiki ni wapi zinakokwenda.

Alipaswa awaambie kuhusu madai kwamba alitumia shirika hilo pia kuombea kiwanja cha ujenzi wa hospitali ya umma, gari la wagonjwa na vifaa vingine vya huduma kwa ajili ya jimbo hilo la Arusha Mjini.

Kukimbilia kuwatisha watu kwa yamini kuwa wasinunue magazeti fulani, wasikilize redio fulani au wasiangalie vituo fulani vya televisheni ni harakati za kijinga au wendawazimu wa kufikiri ambao ni ajabu zaidi unapofanywa na Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha siasa na hata kiongozi mwingine yeyote wa umma.

Mbali na Lema, Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alinikumbusha pia tuhuma zake alipodai kuwa chama hicho kinajipanga kumpeleka Ikulu Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa ifikapo mwaka 2015.

Akiandika katika baadhi ya mitandao ya kijamii wiki iliyopita na baadaye kulithibitishia gazeti dada la MZALENDO, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza alieleza kwa kina namna Heche anavyotumiwa na Dk. Slaa ili kuligawa na kulivuruga baraza hilo la vijana wa Chadema kwa ajili ya maslahi yao binafsi. 

Katika kufanya hivyo, Shonza alidai kuwa Dk. Slaa ameidhinisha Heche alipwe mshahara wa shilingi 700,000 kila mwezi kutokana na ruzuku inayotolewa na serikali kwa Chadema, jambo linalokwenda kinyume cha Katiba ya chama hicho kwa sababu anayepaswa kulipwa mshahara namna hiyo ni Katibu Mkuu wa Bavicha na siyo Mwenyekiti wake.

“Kumlipa mshahara Heche ni kuligawa Baraza la Vijana kwa sababu ni ukiukwaji wa Katiba ya chama…Ni wazi (kwamba) anamlipa fadhila kwa yale aliyofanya ya kuendesha baraza kwa misingi ya kauli za Katibu Mkuu”, anasema Shonza katika taarifa yake hiyo na kumshutumu kwa kuingiza ukanda na ukabila ndani ya Chadema.

Mbali na tuhuma za mshahara, Shonza pia anasema Dk. Slaa aliidhinisha kuwa Heche alipwe shilingi 2,000,000 za pango la nyumba aliyotafutiwa na Chadema baada ya kuwa Mwenyekiti wa Bavicha.

Hatua hiyo inatajwa kuwa inawabagua viongozi wa Bavicha kimatabaka ambapo Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na wengine wote hawana umuhimu, na kwamba hawaonekani kuwa lolote wala chochote katika chama hicho na huenda hawana faida yoyote kisiasa.

Mlolongo wa tuhuma hizo pia unagusia gari aina ya Nissan Patrol lenye rangi nyekundu linalodaiwa kutolewa kwa Bavicha na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Tanzania Bara), lakini katika hali ya ufisadi, Makamu Mwenyekiti huyo anasema lilichukuliwa na Heche anayelitumia kwa shughuli zake mwenyewe huku dereva wake akitajwa kuwa ni mdogo wake.

Katika hali hiyo, sishangai hata kidogo kumuona kijana huyo akitangaza mkutanoni kuwa Dk. Slaa ndiye mgombea urais wa Chadema mwaka 2015 kinyume cha Katiba, kanuni na taratibu nyingine za kawaida za kichama.

Anafanya hivyo ili kuthibitisha tuhuma za Shonza dhidi yake kuwa kuna mchezo ‘mchafu’ ambao unaendelea kati yake na Dk. Slaa huku viongozi wengine wa Bavicha wakitengwa.

Wanalipana fadhila kutokana na kazi wanazopeana kwa ajili ya maslahi yao na siyo kwa faida ya chama wala wanachama, viongozi au wafuasi wa Chadema kama taasisi ila kama kampuni binafsi au Shirika Lisilokuwa la Kiserikali (NGO) linalomilikiwa na familia ama watu wenye malengo wanayoyajua wenyewe.

Bila ya kujali kuwa ni ndani ya Chadema na hata vinginevyo sehemu zote duniani, hakuna Mwenyekiti awe wa NGO, chama cha siasa wala taasisi yoyote na hata vitengo vyake anayelipiwa pango la nyumba au kupewa mshahara ila wote wanapata posho za vikao peke yake, safari ama za uwajibikaji pale wanapokuwa katika kazi zinazotajwa na Katiba za taasisi zao.

Hawalipiwi kodi iwe ya pango ama nyingine yoyote wala kupewa mishahara kwa vile kazi zote zinazohusu uenyekiti haziwi za ajira isipokuwa kujitolea, hivyo haiwezekani Heche afanyiwe kinyume chake endapo siyo rushwa ya kisiasa anayopewa ili naye pia ‘amlinde’, amtetee au kumuunga mkono kwa nguvu zake zote Dk. Slaa. 

Aliposema kuwa anakusudia kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kama chama chake kitampitisha, Zitto alikemewa kwa nguvu nyingi na viongozi wake waliodai kwamba muda wa kutangaza jambo hilo bado haujafika na hata kukaribia pekee.

Alikaripiwa na mwasisi wa Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa Mstaafu wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei na hata Mwenyekiti wa Taifa sasa, Freeman Mbowe na pia Dk. Slaa kwa ulimi wake mwenyewe.

Kinachonishangaza sana ni ukweli kwamba Zitto hakutangaza kuwa yeye ndiye mgombea urais wa chama hicho wakati huo, badala yake alichosema ni kwamba ataomba ridhaa ya kufanya hivyo kwa kuzingatia Katiba ya Chadema, kisha akaomba Mungu akubaliwe na wenzake ili akiipata nafasi hiyo aitumie vizuri kuiongoza Tanzania kwa jinsi inavyopaswa.

Tofauti na kijana huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa muhula wa pili sasa, Heche yeye ametangaza rasmi kuwa katika uchaguzi huo mkuu ujao, mgombea urais wa Chadema atakuwa ni babu huyo wa Karatu aliyetelekeza mkewe na watoto wake.

Amefanya hivyo kwa sababu huenda ndiyo makubaliano waliyofikia kwamba yeye alipiwe pango la nyumba, apewe mshahara huo mnono kinyume cha Katiba ya Chadema na ahodhi gari lililotolewa na Zitto kwa ajili ya Bavicha, lakini naye katika upande wa pili apambane kikamilifu kuhakikisha kuwa Dk. Slaa ndiye anagombea urais mwaka 2015.

Wamelishana yamini kwamba kila mmoja amtumikie mwenzie, hivyo haishangazi kuwa Heche aliamua kumtangaza hadharani mkutanoni babu huyo wa Karatu kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi huo mkuu wa rais, wabunge na madiwani; halafu haijalishi kama alikwenda kinyume cha Katiba, kanuni na taratibu nyingine za Chadema.

Alifanya hivyo sambamba na Lema ambaye aliwalisha yamini wafuasi wake ili wayasusie magazeti yale, televisheni zile pamoja na redio ile kwa sababu wote ninadhani kuwa akili zao za kisiasa ni za kishamba, kilimbukeni na ovyo, na kwamba inawezekana upeo wao wa kupembua mambo ya utawala na uongozi wa umma ni mdogo sana.

Ndiyo maana licha ya kuwa kwao wote ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, lakini akili zao bado ni sawa na za watoto wa chekechea, hatua inayosababisha waseme chochote, wakati wowote na mahali popote bila ya kujali ama kufahamu kwamba athari zake kwao au kwa umma ni kubwa kupindukia!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa e-mail: mimi.mimi011@yahoo.com

Lema anapiga marufuku wananchi kupata habari?

  Lema anapiga marufuku  wananchi kupata habari? o Heche naye aonyesha anavyotumiwa na Dk. Slaa Na Charles Charles MBUNGE wa Aru... [Read More]