• CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM CHAMA MAKINI KINACHOFANYA MAAMUZI KWA VIKAO RASMI
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA

Serikali haiongozwi kwa shinikizo, vitisho vya M4C

 







Na Charles Charles

JUMANNE ya wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kitautumia mwaka 2013 ili kufanya vurugu na kueneza uzushi, uongo, fitina, umbeya, uchochezi pamoja na kuwapandikizia hasira na chuki wananchi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na serikali yake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Mbowe aliyekuwa akiwatangazia maazimio makubwa yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana hivi karibuni, alisema “mwaka 2013 ni wa vitendo”, hivyo hakuna Mtanzania atakayepumua wala kulala kwa vile madai yao mengi kwa Rais hayajatekelezwa!

Machache kati yake ni kutaka iundwe Tume Maalum ya Kimahakama ili ichunguze mauaji kadhaa yaliyotokea nchini ambayo wanadai yana utata, kisha iwachukulie hatua watu wote watakaobainika kuhusika nayo, jambo alilosema kwamba halijafanywa. 

“Binafsi nimekutana na Rais Kikwete na kuzungumza naye kuhusu suala hili, lakini umepita mwezi (mzima) hadi sasa hakuna majibu yoyote”, alisema Mbowe kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Katika hali hiyo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema Kamati Kuu ya Chadema imeamua kwamba Rais akumbushiwe tena, lakini kama ataendelea kunyamaza atalazimishwa kutekeleza matakwa yote hayo kwa namna nyingine, ile ambayo itakuwa ni ya maandamano ya vurugu, ghasia pamoja na mikutano iliyojaa aina zote za uchochezi kwa kutumia kisingizio cha Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) ili kushinikiza afanye wanavyotaka.

Mbali na mpango huo ‘mchafu’, Mbowe alieleza pia kuwa chama chake kitatumia ubabe ili kushinikiza ufanyike uchaguzi mdogo kwa maeneo yote aliyodai yapo wazi katika ngazi za serikali za mitaa, vijiji, vitongoji na kata.

“(Kwa) kawaida maeneo yenye migogoro ya uchaguzi yakiwa wazi ndani ya siku 90, Tume ya Taifa ya Uchaguzi huwa inatangaza uchaguzi (mpya), lakini kuna zaidi ya kata 15 hadi leo na uchaguzi haujafanyika. Tunasema (kuwa) mwakani kata zote hizo hazitatawalika”, alisema.

Akihutubia jijini Dar es Salaam wakati wa kutunuku nishati ya daraja la kwanza ya taifa ya Vladimir Ilyaski Lenin iliyotolewa na serikali ya Urusi kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1986, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wakati huo), Alhaji Ali Hassan Mwinyi alisema:

“Hata Vitabu Vitukufu vya dini vimeandika kuwa ukiona ubaya wowote unatokea mbele yako huna budi kuuzuia kwa mikono yako mwenyewe. Kama huwezi inabidi uukemee kwa ulimi wako mwenyewe, lakini kama huwezi pia angalau basi uukasirikie tu”.

Hivyo ndivyo mimi ninavyotaka kufanya dhidi ya vurugu, fitina, uchochezi pamoja na nia mbaya ya Chadema ya kutaka kuwapandikizia hasira, uzushi, uongo, umbeya, uzandiki na chuki wananchi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na serikali yake nzima. Ninataka kuukemea uovu wote huo kwa mikono yangu mwenyewe kwa njia hii ya makala.

Sitaki kushiriki katika kufanikisha uovu huo unaolenga kuitumbukiza nchi yangu Tanzania katika dimbwi la machafuko yanayoweza kupelekea umwagaji damu mkubwa, kuhasimiana miongoni mwa wananchi na kuchukiana kwa misingi ya itikadi za kisiasa na kutaka amani iliyopo isambaratike kwa namna moja ama nyingine.

Sitaki kuiona Tanzania yangu ikitumbukizwa kwenye lindi la machafuko ya kidini, siasa wala namna nyingine yoyote ile kutokana na ‘ulevi’ tu wa kijinga unaofanywa na baadhi ya watu wenye malengo ‘machafu’, wale ambao kuna wengine wanakwenda mbali zaidi kwa kumtisha Rais eti kuwa asipotekeleza matakwa yao watafanya kila wanavyoweza ili mwaka 2013 nchi yetu isitawalike iwe kisiasa na hata vinginevyo!

Ibara ya 37(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika hivi sasa inasema, nami nanukuu:

“Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote” (mwisho wa kunukuu).

Aidha, Ibara ya 38(1) ya Katiba hiyohiyo inasema kuwa “Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa sheria itakayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge kwa kufuata masharti ya Katiba hii”.

Katika ibara zote hizo, wapi panaposema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analazimika kutekeleza matakwa ya Mbowe au ya Kamati Kuu ya Chadema, na kwamba asipofanya hivyo atatishwa, kushinikizwa au kulazimishwa kwa vurugu za M4C?

Mbowe anapodai kwamba amekutana na kuongea na Rais Kikwete kuhusiana na maombi ya Chadema ya kutaka aunde Tume Maalum ya Kimahakama ili pamoja na mambo mengine, ichunguze mauaji mbalimbali yaliyotokea nchini na kuwachukulia hatua ambao watabainika kuhusika nayo haina maana kuwa lazima afanye wanavyotaka.

Haimaanishi hata kidogo kuwa inabidi Rais avunje Ibara ya 37(1) ya Katiba ya nchi hii, sheria zake, kanuni au taratibu nyingine zote na kufanya jinsi alivyoelekezwa na Mbowe au kuombwa kwa namna yoyote ile na Kamati Kuu ya Chadema.

Haiwezekani kwamba nchi yetu iongozwe kwa matakwa ya chama hicho cha siasa ambacho kwanza hakina ridhaa yoyote ya kuongoza serikali baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2010. Haiwezekani hivi leo viongozi wake watuanzishie mtindo wa kumtishia Rais wetu aliyechaguliwa kwa mujibu wa Ibara ya 38(1) ya Katiba ili kukidhi matkwa yao wenyewe.

Mauaji yenyewe wanayojifaragua nayo kutaka yaundiwe Tume Maalum ya Kimahakama ya kuyachunguza tayari yanashughulikiwa kwa kuzingatia Ibara ya 108(1) ya Katiba hiyohiyo, lakini wanacholenga hasa ni kutaka kuficha uovu wao wenyewe kwa vile yote yalitokana na vurugu zao, fujo zao, ubabe wao na kutotaka kutii sheria za nchi.

Ni wao walianzisha vurugu kwa kutaka kutaka mpaka Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Arusha Januari 5, 2011 na kulazimisha Jeshi la Polisi litumie nguvu za ziada kuwatawanya ili kukiokoa, vinginevyo walikuwa wakilenga kukiteka ili waibe silaha zote zilizokuwemo, kuwafungulia mahabusu wote waliokuwa wakishikiliwa humo wakiwemo watuhumiwa wa mauaji, ujambazi wa aina zote na kadhalika.

Walikuwa tayari wameshachoma vibanda kadhaa vya biashara barabarani ambavyo wamiliki wake walikataa katakata kuwaunga mkono katika vurugu zao, na pia walipiga magari mawe na kuyavunjavunja vioo, jambo ambalo pia walikuwa wamelifanya dhidi ya Jengo la Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Mkoa wa Arusha.

Jaribio la kukiteka kituo hicho cha polisi lilikuwa la mwisho na madhara yake yangekuwa ni makubwa kupindukia, hivyo ndiyo maana jeshi hilo lililazimika kuwarushia risasi za moto baada ya awali kuzielekeza hewani ili kuwatishia, lakini wakabaki wanasonga mbele kwa hamasa iliyokithiri kwa uovu wote huku wakiwa tayari kumwaga damu kwa silaha za jadi yakiwemo mawe, bisibisi na majambia.

Kama polisi wasingelazimika kuwapiga risasi na kuwaua watatu huku wengine wakiachwa na majeraha hakika silaha zote za kivita zilizokuwemo kituoni wangezipora, hatua ambayo hakuna asiyejua nini kililengwa hasa ukizingatia ukweli kwamba wana agenda nyingine ya kijinai ya kutaka kuitenga mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro na kuanzisha Jamhuri ya Kaskazini!

Julai 14, mwaka huu, viongozi na wafuasi wa Chadema walihusika kwa namna moja ama nyingine na mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Kata ya Ndago, Iramba mkoani Singida, Yohana Mpinga.

Kutoka huko walihamishia uhalifu wao huo mjini Morogoro ambako pia walisababisha kifo cha kijana mmoja, mauaji yaliyofuatiwa na mengine tena katika kijiji cha Nyororo, wilaya ya Mufindi, Iringa hapo Septemba 2, wakati vurugu zao ziliposababisha kupigwa risasi kwa aliyekuwa mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten wa mkoa huo, Daud Mwangosi na kufa papo hapo.

Kama nilivyosema, mauaji hayo yote yanashughulikiwa na vyombo vinavyohusika. Tayari watuhumiwa wanakabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 59B(1) – (5) na 108(1) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo wanaosema vinginevyo au kumlazimisha Rais Kikwete atende kinyume chake ni kama wendawazimu wa kufikiri.

Kuhusu kisingizio kingine cha kutaka kufanya uvurugu ili mwaka 2013 Tanzania isitawalike kwa sababu ya kushinikiza chaguzi ndogo za udiwani, serikali za mitaa, vijiji na vitongoji huo pia ni ujinga wa akili kichwani.

Ibara ya 74(6)(a) – (e) ya Katiba ya nchi inayataja majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba ni pamoja kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge katika Jamhuri ya Muungano.

Mengine ni kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa rais na wabunge, kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge na, kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge.

Kana kwamba haitoshi, Kifungu Kidogo cha 11 cha Ibara hiyo kinasema “katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya serikali au maoni ya chama chochote cha siasa”.

Katika hali hiyo, dhamira ya Chadema ya kutaka kuilazimisha kwa vurugu za M4C kwamba itekeleze matakwa ya chama hicho katika kujaza nafasi zilizo wazi za udiwani, inakwenda kinyume cha Ibara ya 74(11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni juhudi za kutaka kufanya ghasia zinazolenga kusababisha umwagaji damu nchini siyo kwa sababu kuna jambo lololte lililokwenda kinyume cha Katiba au sheria yoyote ya nchi hii. 

Ni harakati za makusudi zinazolenga kuifanya Tanzania iwe kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Nigeria, Somalia, Sudan Kaskazini, Sudani ya Kusini, Libya, Misri, Tunisia, Irak, Afghanistani, Pakistani, Palestina, Israeli, Lebanon na kadhalika ambako umwagaji wa damu kutokana na sababu za kisiasa, tofauti za kidini au za kijadi na upumbavu mwingine ni suala la kawaida.

Sitaki Tanzania ifanane kwa namna yoyote ile na taifa lolote kati ya hayo kutokana na tamaa tu za kijinga walizonazo viongozi wa Chadema, vibaraka wao, wapambe wao, mabwana zao na hata vinginevyo.

Sitaki Rais alazimishwe kuvunja sheria wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili awaridhishe wendawazimu wachache tu kwa faida zao wenyewe, wale ambao wapo radhi na tayari kuona mwaka ujao nchi yetu haitawaliki mpaka matakwa yao kwanza yatekelezwe. 

Namshukuru kwa namna zote Rais Kikwete aliyegoma katakata kulazimishwa na viongozi wa Chadema kufanya wanavyotaka, msimamo ambao naamini kamwe hauwezi ukayumba hata iweje.

Atabaki nao wakati wote wa utawala wake na mahali popote, ukweli ambao uko hivyo kwa sababu serikali haiongozwi kwa shinikizo wala vitisho vya maandamano ya vurugu za M4C ila kwa matakwa ya sheria na Katiba ya nchi hii.

Mungu Ibariki Afrika. Mungu Ibariki Tanzania!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa e-mail: mimi.mimi011@yahoo.com

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Hakuna mwanaume changudoa kama Charles Charles kihiyo aliyeghushi cheti cha fomu four. Jamaa anaendekeza njaa kujifanya mwandishi wa habari wakati si chochote si lolote bali njaa. Mbona hasemi ukweli kuwa alikuwa mwanachama wa CHADEMA? Kijana huyu mwana haramu asiye na baba anakera Mungu anajua. Charles acha uchangudoa uanze kufikiri kuishi bila kutegemea uongo, kughushi, unafiki na kujikomba kama changudoa.

Leave a Reply