• CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM CHAMA MAKINI KINACHOFANYA MAAMUZI KWA VIKAO RASMI
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAJUMBE WA NEC, 25/9/2012, KABLA YA KIKAO KILICHOFANYIKA MJINI DODOMA, KUTEUA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA. PICHA: BASHIR NKOROMO
  • CHAMA CHA MAPINDUZI

    CCM NDICHO CHAMA CHA SIASA KINACHOONGOZA KWA KUWA NA WAFUASI WENGI TANZANIA

Wanaompachika urais Dk. Slaa kupitia ‘Jamii Forums’ wanamtafutia maradhi







Na Charles Charles

MOJA kati ya hadithi nzuri kabisa za kuchekesha zilizosimuliwa mapema wiki hii ni ile iliyosema kuwa “Dk. Slaa kinara wa urais (mwaka) 2015”. Niliisoma na kuirudia mara mbili nikilenga niilewe kwa uhakika, mwisho nikakumbuka nyingine iliyowahi pia kufanana kama hiyo.

“Wakati mjadala wa nani anafaa kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unashika kasi kila kona ndani na nje ya nchi, jina la Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa limeng’ara”, liliandika gazeti moja la kila siku nchini, Jumatano wiki hii na kuendelea:

“…Kwa mujibu wa kura za maoni zilizoendeshwa na mtandao maarufu duniani wa Jamii Forums kwa kuuliza: “Nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema na CCM”, majina manne yalipambanishwa, mawili kutoka CCM na mawili Chadema”.

Mchanganuo wa kura hizo ambazo hata hivyo hazihusiani chochote na uchaguzi wowote wa rais ila kama za maoni ya ndani ya vyama hivyo vyenyewe, zoezi ambalo pia lilijaa ushabiki binafsi kwa watu waliohusishwa zilimpa ‘ushindi’ Dk. Slaa dhidi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ingawa mchezo huo si lolote wala chochote kisiasa kwa yeyote kati yao.

“Jumla ya wapiga kura 1,188 walishiriki kuwapigia kura wagombea wa Chadema”, inasema habari hiyo na kuongeza: “Dk. Slaa alipigiwa kura 1,007, sawa na asilimia 84.76 wakati Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliibuka na kura 181, sawa na asilimia 15”.

Mbali na hao, wengine ‘waliopambanishwa’ lakini kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.

Katika hadithi hiyo ya kitoto, jumla ya kura walizopigiwa zimetajwa kuwa 375 na Lowassa kupewa 164 zilizotajwa kuwa ni asilimia 43.73, kisha Membe akaishia 67 ambazo ni sawa na asilimia 17.87 tu.

“Matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa Dk. Slaa aliibuka na ushindi mkubwa wa kura 1,007 kwa kupigiwa kura nyingi zaidi kuliko majina ya washiriki wengine waliopendekezwa na kuingia katika mnyukano huo. Mshindi wa pili ni Zitto mwenye kura 181, wa tatu Lowassa mwenye kura 164 na Membe anashika nafasi ya nne kwa kura 67”, inabainishwa.

Nimeanza makala yangu kwa kusema hii ni hadithi ya kuchekesha kutokana na malengo ya makusudi ambayo ni mawili.

Kwanza ni kuanza kumpigia debe la waziwazi Dk. Slaa ili ateuliwe kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya Chadema mwaka 2015 dhidi ya Zitto, jambo linalofanywa baada ya mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kusema hadharani kwamba anataka kufanya hivyo wakati huo.

Ni juhudi za makusudi zilizopangwa na kutekelezwa na kikosi cha wapambe wanaotarajia mkakati wao utasaidia kumjenga katika chama chake, na pili wanaamini kuwa njia hiyohiyo itamaliza kabisa ndoto zote alizonazo Zitto na pia kumsambaratisha hata mwenyewe kisiasa.

Wapambe hao wa padri huyo wa zamani wanadhani kwa kufanya hivyo atapata umaarufu nje na ndani ya chama chake, jambo ambalo mtu yeyote asiyekuwa na mtindio wa ubongo haliwezi kumuingia kichwani ila kama ni mtoto wa chekechea.

Ni mchezo uliotengenezwa kipuuzi kwa ajili ya watu wapuuzi wanaoweza wakaaminishwa upuuzi na siyo wenye akili timamu hata kama ni washamba wa kufikiri. Hakuna anayeweza kurubuniwa kwa ujinga uliotengenezwa maalum ili kumfariji babu huyo wa watu. Ni juhudi zinazofanywa pia ili kumfariji baada ya kusambaratishwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kutamka kwamba hayatambui matokeo.

Ni juhudi zinazofanywa kwa makusudi ili kumpunguzia hasira ambapo alifikia mpaka hatua ya kutishia kuwa Tanzania isingeweza kutawalika “mpaka kieleweke”, lakini pia ni harakati za kutaka kumfariji kwa sababu bado ‘amechanganyikiwa’ kichwani, halafu wapambe wake wanafahamu kwamba uwezo wake wa kutathmini au kuchanganua mambo ni mdogo sana.

Ndiyo maana kwa mfano huwezi kuzichanganya kura za urais wa Madagascar na Cameron au za Kenya na Msumbiji. Haiwezekani kura za maoni za kutafuta mgombea urais, ubunge ama udiwani za ndani ya CCM zichanganywe na kura kama hizo za Chadema kwa sababu hakuna uhusiano wowote uliopo kati yake.

Gazeti hilo lenyewe limeeleza kuwa Dk. Slaa alipambanishwa na Zitto katika chama chao,  halafu Lowassa naye alikutanishwa na Membe kama wana CCM. Katika hali hiyo na hata vinginevyo, haiwezekani kuja kuyachanganya pamoja matokeo ya kura zao maana hayana uhusiano wowote na katika hali zote.

Mbali na kutaka kumdanganya kwa sababu wanafahamu kuwa uwezo wake wa kuchanganua mambo ni mdogo, wapo waliolenga kumtisha Zitto kwa imani kwamba atahofia kushindwa katika mbio hizo na kuamua kuachana nazo.

Walilenga kumtisha kwamba endapo ameungwa mkono na watu 181 tu kati ya 1,188 walioshiriki zoezi hilo huku Dk. Slaa akikubaliwa na 1,007 katika hesabu hiyo, mwaka 2015 anaotaka kugombea urais ataishia kuaibika, hivyo ili asitumbukie kwenye aibu hiyo inabidi apime mwenyewe, atathmini na kujitoa.

Ndivyo pia walivyolenga dhidi ya CCM kutaka ionekane kwamba imechuja huku Chadema yao ikimeremeta katika kipindi hiki cha mpito kuelekea mwaka 2015. Pamoja na hayo na hata vinginevyo, hesabu inayochezwa ni kama ngoma ya kitoto ambayo siku zote haikeshi.

Kama nilivyobainisha tokea mapema huo ni ujinga wa kufikiri kwa sababu hakuna asiyejua kwamba katika uchangiaji unaofanyika katika mitandao kama Jamii Forums, mtu mmoja anaweza kujiita majina hata 20, 50, 80 au zaidi yake. Inategemea na jinsi anavyopata nafasi ya kuchangia chochote, na pia kuna wengine wanaodhani kuwa njia hiyo ni bira zaidi kisiasa kama Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa wa Chadema, John Mnyika.

Kwa mfano hata Dk. Slaa mwenyewe pia anaweza kujiita Athumani, Saidi, Yohana, Richie, Danford, Khadija, Hilda, Rhoda, Fatuma, Lucy na kadhalika. Anaweza kujipachika kila aina ya majina ili hatimaye ajipigie kura, kazi amabyo pia inaweza ikafanywa na wapambe wake ama kwa makubaliano naye maalum au kwa kujipendekeza wenyewe.

Ndiyo maana tunadanganywa pia kuwa eti mtandao huo ni “maarufu duniani” kote wakati hakuna ukweli. Hauna umaarufu hata Afrika Mashariki pekee mbali ya Afrika Mashariki na Kati, Afrika iliyopo kusini mwa Jangwa la Sahara ama Afrika peke yake.

Hausomwi hata na watu 3,000 peke yao angalau kwa siku moja ama wiki nzima isipokuwa kikundi ambacho kwa kawaida ni kilekile, tena kilichokusanya kwa kiwango kikubwa zaidi wanachama au wafuasi wa Chadema.

Ni ulimbukeni unaofanana kama ulevi wa pombe ambao kwa mfano wanywaji wa bia aina ya Tusker, Ndovu au Serengeti huwa ni walewale kwa kila siku na mtu mmoja anaweza kumaliza chupa tano, 10 au hata sanduku moja peke yake na kuonekane kuwa ni wengi.

Mtu mmoja ama pengine na mpenzi wake wanaweza wakajifungia mahali wakaanza kuagiza bia mojamoja, mbili au tatu wakishinda mpaka jioni wanaweza kumaliza hata sanduku zima na kadhalika. Hapo huwezi kusema kuwa eti wanywaji wa pombe wanaongezeka kwa kasi ama kila kunapokucha wakati ukweli ni walewale.

Hivyo ndivyo inavyokuwa pia katika mitandao yote ya kijamii ambako mtu mmoja anaweza ‘akaingia’ hata kutwa nzima na hasa anapokuwa na kazi ndogo tu ya kuandika majina kama “DK. SLAA, ZITTO, LOWASSA” au “MEMBE”.  

Anaweza akafanya hivyo kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manane ili ‘kumbeba’ mtu wake au kwa kujipigia kura mwenyewe akibadili majina kuanzia Mayasa, Teophil, Mkunza, Petro, Esther, Augusta, Madaraka na kadhalika ili isionekane kuwa ni yuleyule isipokuwa jopo la watu.

Huo ndio mchezo uliofanyika ili kumbeba Dk. Slaa kwa imani kuwa atashinda urais mwaka 2015 na kwenda Ikulu kwa daraja la Chadema yake.

Mtu yeyote anayebisha haya aende akazunguke katika mitaa yote mijini na vijijini, kisha aulize kuwa ni watu wangapi ‘wanaingia’ katika mitandao kama ya twitter, Jamii Forums, facebook na mengineyo ili aone.

Hata intaneti wanakoshinda hadi watu wasiojua namna gani ya kutumia twitter au facebook nako utakuta wanaokwenda hawazidi hata 40 kwa siku moja. Kule wanakokwenda wengi ni zile zinazokuwa karibu zaidi na vyuo vikuu.

Zinapata watu wengi ambao siku zote huwa wanafunzi wa shahada mbalimbali kwa ajili ya kujitafutia ‘material’, na pili ni zile zinazokuwa jirani na ofisi za vilabu vya waandishi wa habari hususan mikoani.

Wapiga kura walio wengi mijini na vijijini hawajawahi hata kusikia neno “intaneti” na hata mitandao iwe ya twitter, facebook, jamii forums wala mwingine wowote. Hawajui chochote kuhusu mambo hayo yote na ndiyo maana ni ajabu kuitegemea kwa namna yoyote ile kupata ushindi wa urais maana haihusiki nao.

Haiwezi kumfanya Dk. Slaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwe mwaka 2015, 2020, 2025 wala mbele ya safari isipokuwa kama ni serikali ya maigizo kama michezo ya fukuto, radi, ngweso na kadhalika.  

Katika hali hiyo na hata vinginevyo, wote walioshiriki ‘kumrusha roho’ babu huyo wa watu sina ugomvi nao wowote ila ninaomba wauzingatie ushauri wangu huu: waache kumpachika urais wala ushindi wa kupitia mtandao huo wa Jamii Forums kwani hautakuwepo daima.

Waache kabisa kufanya hivyo kwa sababu wanampandikizia imani na ndoto za alinacha. Wanamtafutia maradhi yakiwemo sugu pindi akigombea tena nafasi hiyo na kushindwa maana hataamini masikioni wala machoni.

Mungu Ibariki Tanzania!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Hakuna mwanaume changudoa kama Charles Charles kihiyo aliyeghushi cheti cha fomu four. Jamaa anaendekeza njaa kujifanya mwandishi wa habari wakati si chochote si lolote bali njaa. Mbona hasemi ukweli kuwa alikuwa mwanachama wa CHADEMA? Kijana huyu mwana haramu asiye na baba anakera Mungu anajua. Charles acha uchangudoa uanze kufikiri kuishi bila kutegemea uongo, kughushi, unafiki na kujikomba kama changudoa.

Leave a Reply