Na Charles Charles
MOJA
kati ya hadithi nzuri kabisa za kuchekesha zilizosimuliwa mapema wiki hii ni
ile iliyosema kuwa “Dk. Slaa kinara wa urais (mwaka) 2015”. Niliisoma na kuirudia
mara mbili nikilenga niilewe kwa uhakika, mwisho nikakumbuka nyingine iliyowahi
pia kufanana kama hiyo.
“Wakati
mjadala wa nani anafaa kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
unashika kasi kila kona ndani na nje ya nchi, jina la Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa limeng’ara”, liliandika
gazeti moja la kila siku nchini, Jumatano wiki hii na kuendelea:
“…Kwa
mujibu wa kura za maoni zilizoendeshwa na mtandao maarufu duniani wa Jamii
Forums kwa kuuliza: “Nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya
Chadema na CCM”, majina manne yalipambanishwa, mawili kutoka CCM na mawili
Chadema”.
Mchanganuo
wa kura hizo ambazo hata hivyo hazihusiani chochote na uchaguzi wowote wa rais ila
kama za maoni ya ndani ya vyama hivyo vyenyewe,
zoezi ambalo pia lilijaa ushabiki binafsi kwa watu waliohusishwa zilimpa ‘ushindi’
Dk. Slaa dhidi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ingawa mchezo huo
si lolote wala chochote kisiasa kwa yeyote kati yao.
“Jumla
ya wapiga kura 1,188 walishiriki kuwapigia kura wagombea wa Chadema”, inasema
habari hiyo na kuongeza: “Dk. Slaa alipigiwa kura 1,007, sawa na asilimia 84.76
wakati Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliibuka na kura 181, sawa na asilimia
15”.
Mbali
na hao, wengine ‘waliopambanishwa’ lakini kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Waziri
Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa pamoja na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.
Katika
hadithi hiyo ya kitoto, jumla ya kura walizopigiwa zimetajwa kuwa 375 na
Lowassa kupewa 164 zilizotajwa kuwa ni asilimia 43.73, kisha Membe akaishia 67 ambazo
ni sawa na asilimia 17.87 tu.
“Matokeo
ya jumla yanaonyesha kuwa Dk. Slaa aliibuka na ushindi mkubwa wa kura 1,007 kwa
kupigiwa kura nyingi zaidi kuliko majina ya washiriki wengine waliopendekezwa
na kuingia katika mnyukano huo. Mshindi wa pili ni Zitto mwenye kura 181, wa
tatu Lowassa mwenye kura 164 na Membe anashika nafasi ya nne kwa kura 67”, inabainishwa.
Nimeanza
makala yangu kwa kusema hii ni hadithi ya kuchekesha kutokana na malengo ya
makusudi ambayo ni mawili.
Ni
juhudi za makusudi zilizopangwa na kutekelezwa na kikosi cha wapambe wanaotarajia
mkakati wao utasaidia kumjenga katika chama chake, na pili wanaamini kuwa njia
hiyohiyo itamaliza kabisa ndoto zote alizonazo Zitto na pia kumsambaratisha hata
mwenyewe kisiasa.
Wapambe
hao wa padri huyo wa zamani wanadhani kwa kufanya hivyo atapata umaarufu nje na
ndani ya chama chake, jambo ambalo mtu yeyote asiyekuwa na mtindio wa ubongo
haliwezi kumuingia kichwani ila kama ni mtoto wa chekechea.
Ni
mchezo uliotengenezwa kipuuzi kwa ajili ya watu wapuuzi wanaoweza wakaaminishwa
upuuzi na siyo wenye akili timamu hata kama ni
washamba wa kufikiri. Hakuna anayeweza kurubuniwa kwa ujinga uliotengenezwa maalum
ili kumfariji babu huyo wa watu. Ni juhudi zinazofanywa pia ili kumfariji baada
ya kusambaratishwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kutamka kwamba
hayatambui matokeo.
Ni
juhudi zinazofanywa kwa makusudi ili kumpunguzia hasira ambapo alifikia mpaka
hatua ya kutishia kuwa Tanzania isingeweza kutawalika “mpaka kieleweke”, lakini
pia ni harakati za kutaka kumfariji kwa sababu bado ‘amechanganyikiwa’ kichwani,
halafu wapambe wake wanafahamu kwamba uwezo wake wa kutathmini au kuchanganua mambo
ni mdogo sana.
Ndiyo
maana kwa mfano huwezi kuzichanganya kura za urais wa Madagascar na Cameron au za Kenya na Msumbiji. Haiwezekani kura
za maoni za kutafuta mgombea urais, ubunge ama udiwani za ndani ya CCM
zichanganywe na kura kama hizo za Chadema kwa
sababu hakuna uhusiano wowote uliopo kati yake.
Gazeti
hilo lenyewe limeeleza kuwa Dk. Slaa alipambanishwa
na Zitto katika chama chao, halafu
Lowassa naye alikutanishwa na Membe kama wana
CCM. Katika hali hiyo na hata vinginevyo, haiwezekani kuja kuyachanganya pamoja
matokeo ya kura zao maana hayana uhusiano wowote na katika hali zote.
Mbali
na kutaka kumdanganya kwa sababu wanafahamu kuwa uwezo wake wa kuchanganua
mambo ni mdogo, wapo waliolenga kumtisha Zitto kwa imani kwamba atahofia
kushindwa katika mbio hizo na kuamua kuachana nazo.
Walilenga
kumtisha kwamba endapo ameungwa mkono na watu 181 tu kati ya 1,188 walioshiriki
zoezi hilo huku Dk. Slaa akikubaliwa na 1,007 katika hesabu hiyo, mwaka 2015 anaotaka
kugombea urais ataishia kuaibika, hivyo ili asitumbukie kwenye aibu hiyo
inabidi apime mwenyewe, atathmini na kujitoa.
Ndivyo
pia walivyolenga dhidi ya CCM kutaka ionekane kwamba imechuja huku Chadema yao ikimeremeta katika
kipindi hiki cha mpito kuelekea mwaka 2015. Pamoja na hayo na hata vinginevyo,
hesabu inayochezwa ni kama ngoma ya kitoto
ambayo siku zote haikeshi.
Kama
nilivyobainisha tokea mapema huo ni ujinga wa kufikiri kwa sababu hakuna
asiyejua kwamba katika uchangiaji unaofanyika katika mitandao kama
Jamii Forums, mtu mmoja anaweza kujiita majina hata 20, 50, 80 au zaidi yake.
Inategemea na jinsi anavyopata nafasi ya kuchangia chochote, na pia kuna
wengine wanaodhani kuwa njia hiyo ni bira zaidi kisiasa kama
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa wa Chadema, John Mnyika.
Kwa
mfano hata Dk. Slaa mwenyewe pia anaweza kujiita Athumani, Saidi, Yohana, Richie,
Danford, Khadija, Hilda, Rhoda, Fatuma, Lucy na kadhalika. Anaweza kujipachika
kila aina ya majina ili hatimaye ajipigie kura, kazi amabyo pia inaweza
ikafanywa na wapambe wake ama kwa makubaliano naye maalum au kwa kujipendekeza
wenyewe.
Ndiyo
maana tunadanganywa pia kuwa eti mtandao huo ni “maarufu duniani” kote wakati hakuna
ukweli. Hauna umaarufu hata Afrika Mashariki pekee mbali ya Afrika Mashariki na
Kati, Afrika iliyopo kusini mwa Jangwa la Sahara
ama Afrika peke yake.
Hausomwi
hata na watu 3,000 peke yao
angalau kwa siku moja ama wiki nzima isipokuwa kikundi ambacho kwa kawaida ni
kilekile, tena kilichokusanya kwa kiwango kikubwa zaidi wanachama au wafuasi wa
Chadema.
Ni
ulimbukeni unaofanana kama ulevi wa pombe ambao kwa mfano wanywaji wa bia aina
ya Tusker, Ndovu au Serengeti huwa ni walewale kwa kila siku na mtu mmoja
anaweza kumaliza chupa tano, 10 au hata sanduku moja peke yake na kuonekane kuwa
ni wengi.
Mtu
mmoja ama pengine na mpenzi wake wanaweza wakajifungia mahali wakaanza kuagiza bia
mojamoja, mbili au tatu wakishinda mpaka jioni wanaweza kumaliza hata sanduku zima
na kadhalika. Hapo huwezi kusema kuwa eti wanywaji wa pombe wanaongezeka kwa
kasi ama kila kunapokucha wakati ukweli ni walewale.
Hivyo
ndivyo inavyokuwa pia katika mitandao yote ya kijamii ambako mtu mmoja anaweza ‘akaingia’
hata kutwa nzima na hasa anapokuwa na kazi ndogo tu ya kuandika majina kama “DK. SLAA, ZITTO, LOWASSA” au “MEMBE”.
Anaweza
akafanya hivyo kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manane ili ‘kumbeba’ mtu wake au kwa
kujipigia kura mwenyewe akibadili majina kuanzia Mayasa, Teophil, Mkunza, Petro,
Esther, Augusta, Madaraka na kadhalika ili isionekane kuwa ni yuleyule
isipokuwa jopo la watu.
Huo
ndio mchezo uliofanyika ili kumbeba Dk. Slaa kwa imani kuwa atashinda urais
mwaka 2015 na kwenda Ikulu kwa daraja la Chadema yake.
Mtu
yeyote anayebisha haya aende akazunguke katika mitaa yote mijini na vijijini, kisha
aulize kuwa ni watu wangapi ‘wanaingia’ katika mitandao kama ya twitter, Jamii
Forums, facebook na mengineyo ili aone.
Hata
intaneti wanakoshinda hadi watu wasiojua namna gani ya kutumia twitter au
facebook nako utakuta wanaokwenda hawazidi hata 40 kwa siku moja. Kule wanakokwenda
wengi ni zile zinazokuwa karibu zaidi na vyuo vikuu.
Zinapata
watu wengi ambao siku zote huwa wanafunzi wa shahada mbalimbali kwa ajili ya kujitafutia
‘material’, na pili ni zile zinazokuwa jirani na ofisi za vilabu vya waandishi
wa habari hususan mikoani.
Wapiga
kura walio wengi mijini na vijijini hawajawahi hata kusikia neno “intaneti” na
hata mitandao iwe ya twitter, facebook, jamii forums wala mwingine wowote.
Hawajui chochote kuhusu mambo hayo yote na ndiyo maana ni ajabu kuitegemea kwa
namna yoyote ile kupata ushindi wa urais maana haihusiki nao.
Haiwezi
kumfanya Dk. Slaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwe mwaka 2015, 2020, 2025 wala mbele
ya safari isipokuwa kama ni serikali ya maigizo kama
michezo ya fukuto, radi, ngweso na kadhalika.
Katika
hali hiyo na hata vinginevyo, wote walioshiriki ‘kumrusha roho’ babu huyo wa
watu sina ugomvi nao wowote ila ninaomba wauzingatie ushauri wangu huu: waache
kumpachika urais wala ushindi wa kupitia mtandao huo wa Jamii Forums kwani hautakuwepo
daima.
Waache
kabisa kufanya hivyo kwa sababu wanampandikizia imani na ndoto za alinacha.
Wanamtafutia maradhi yakiwemo sugu pindi akigombea tena nafasi hiyo na
kushindwa maana hataamini masikioni wala machoni.
Mungu
Ibariki Tanzania!
Hakuna mwanaume changudoa kama Charles Charles kihiyo aliyeghushi cheti cha fomu four. Jamaa anaendekeza njaa kujifanya mwandishi wa habari wakati si chochote si lolote bali njaa. Mbona hasemi ukweli kuwa alikuwa mwanachama wa CHADEMA? Kijana huyu mwana haramu asiye na baba anakera Mungu anajua. Charles acha uchangudoa uanze kufikiri kuishi bila kutegemea uongo, kughushi, unafiki na kujikomba kama changudoa.